Home Azam FC BAADA YA KUSOMA MAZINGIRA….WACOLOMBIA WA AZAM FC NI MOTO NA NUSU…BALAA LAO...

BAADA YA KUSOMA MAZINGIRA….WACOLOMBIA WA AZAM FC NI MOTO NA NUSU…BALAA LAO SIO POA..

Habari za Michezo

Azam FC ina hatari! Kwa sasa ipo kambini ikiendelea kujifua kwa ajili ya mechi zijazo, lakini cha kufurahisha zaidi kikosini kwa sasa kuna mastaa wawili raia wa Colombia ambao wanasikilizia Ligi Kuu ianze waonyeshe ufundi.

Wachezaji hao ni straika Franklin Navarro (24), aliyesajiliwa akitokea Inter Palmira na beki wa kati Yeison Fuentes (21), aliyetokea Leones FC zote za nchini kwao na wametua Azam katika dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 15.

Navarro na Yeison wameingia kwenye usajili wa Azam sawa na kipa Msudani Mohammed Mustafa akichukua nafasi ya makipa wawili Ali Ahmada na Abdulai Iddrisu walio majeruhi, huku Wacolombia wakichukua nafasi ya straika Idris Mbombo aliyeachwa na kusajiliwa na Nkana ya Zambia.

Kocha mkuu wa Azam, Youssouph Dabo aliwasifu wawili hao kuwa wachezaji wazuri na wanaendelea na mazoezi wakisubiri ligi ianze waonyeshe walicho nacho.

“Ni wachezaji wazuri na tupo nao mazoezini. Kinachofanyika kwa sasa ni kujenga timu yenye umoja na ushirikiano huku tukisubiri ligi ianze kila mmoja aonyeshe uwezo wake kwenye mechi za ushindani,” alisema Dabo.

Azam ndiyo vinara wa ligi wakiwa na alama 31 walizovuna kwenye mechi 13 wakishinda 10, sare moja na kupoteza mbili na mechi ijayo itakuwa Februari 16 dhidi ya Tanzania Prisons.

SOMA NA HII  MSEMAJI AZAM FC AJIINGIZA KWENYE LIGI YA UBISHANI KUHUSU UWEZO WA MORRISON....ADAI HANA UBORA WOWOTE...