Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO…..YANGA KUWAKOSA MASTAA HAWA SABA…

KUELEKEA MECHI YA KESHO…..YANGA KUWAKOSA MASTAA HAWA SABA…

Habari za Yanga leo

KOCHA wa Yanga, Miguel Gamondi amesema pamoja na kwamba atawakosa mastaa wake kwenye mchezo wa kesho, bado wapo tayari kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

Yanga ambayo ndiyo mabingwa watetezi kesho itashuka uwanjani kumenyana na Hausing FC ya Njombe kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), utakaopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi jijini la Dar es Salaam katika mchezo huo wa hatua ya 64 Bora.

Yanga itaingia uwanjani saa 1:00 bila mastaa wake saba wale waliokuwa kwenye vikosi vyao vya timu za taifa ambao tayari timu zao zimeondolewa hatua ya makundi ambao ni kutoka Taifa Stars na Zambia pamoja na wawili ambao bado wapo kwenye michuano.

Nahodha wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrahim Hamad ‘Bacca’, Mudathir Yahaya na Keneddy Musonda ambao wamepewa mapumziko hadi Jumatano ndiyo watakwenda kambini, huku Aziz Ki na Djigui Diarra wakikosekana kutokana na kuendelea kubaki na timu zao, Burkina Faso na Mali kwenye hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo mikubwa Afrika.

Kwa mujibu wa Gamondi ambaye timu yake inashikilia rekodi ya kutwaa ubingwa huu mara saba tangu mwaka 1967, amesema anatambua umuhimu wa mchezo huo ulio mbele yao lakini anaamini wachezaji waliopo wanaweza kufanya mambo makubwa na kuivusha timu hiyo hatua inayofuata na wala hana wasiwasi .

“Wachezaji waliokuwa timu zao za taifa na wameaga mashindano wataungana na wenzao Jumatano mara baada ya mapumziko ya muda mfupi, nafahamu kuwa wamesafiri kwa umbali mrefu wanatakiwa kupumzika kidogo, kuhusu mchezo wa Jumanne (kesho), natambua umuhimu wake lakini unaweza ukachezwa bila ya hao.

“Yanga ina wachezaji wengi bora, wataifanya kazi kama inavyotakiwa wala hakuna wasiwasi.” alisema kocha huyo ambaye timu yake inashika nafasi ya pili kwenye ligi na pointi 30.

Akizungumzia maandalizi yao kwa ujumla alisema yanakwenda vizuri na wachezaji wapo katika hali nzuri ya ushindani.

“Maandalizi yanakwenda vizuri na kila mchezaji yupo kwenye hali nzuri ya ushindani naamini tutakuwa na mchezo mzuri Jumanne hii ni baada ya maandalizi mazuri, unajua sisi tulianza kujiandaa mapema hivyo tupo tayari kwa ajili ya mechi hii muhimu.” alisema kocha huyo raia wa Argentina aliyejiunga na Yanga akichukua nafasi ya Nasreddine Nabi.

Hata hivyo, pamoja na Yanga kuwakosa mastaa hao saba, bado itakuwa na kikosi kizuri kwa kuwa mastaa kama, Maxi Nzegeli, Pacome Zouzuo, Abuutwalb Mshery, Yao Kouassi, Khalid Aucho, Clement Mzize na Joseph Guede wapo kambini wakijifua kwa ajili ya mchezo huo.

Mechi nyingine za hatua hiyo, Mtibwa itacheza na Nyakangwe saa 10:00, Jumatano Simba itavaana na Tembo, Kagera dhidi ya Dar City

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU