Home Habari za michezo CHAMA, KIBU NA ZIMBWE Jr WALIAMSHA SIMBA HUKO….MABOSI WATAKA HESHIMA TU..

CHAMA, KIBU NA ZIMBWE Jr WALIAMSHA SIMBA HUKO….MABOSI WATAKA HESHIMA TU..

Habari za Simba leo

Tizi la Simba huko Bunju linazidi kunoga baada ya mastaa wa timu hiyo kuendelea kuwasili kambini kujiandaa na mechi zijazo, huku nyota kama Kibu Denis na Clatous Chama wakiitwa fasta Dar es Salaam.

Juzi, Simba ilirejea kambini baada ya mapumziko mafupi ya siku 10 na kuanza tizi la kuweka miili sawa sambamba na gym, huku mastaa wapya Muivory Coast Freddy Michael, na wazawa Edwin Balua, Saleh Karabaka na Ladack Chasambi wakiongeza mzuka kambini.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula alisema kwa sasa kikosi kimetimiua na wanajiandaa kurejesha heshima yao Msimbazi.

“Tumetimia. Kuna wachezaji kocha aliwahitaji na tumewasajili kwenye dirisha dogo. Ukiachana na hao asilimia kubwa waliokuwa Afcon nao wanarejea, hivyo sasa kilichobaki ni kusubiri mechi zianze watu wapate burudani,” alisema Kajula.

Hata hivyo, Mzamiru Yassin, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Aishi Manula na Kibu Denis waliokuwa kwenye timu ya taifa ‘Taifa Stars’ sambamba na Chama aliyekuwa timu ya taifa ya Zambia zilizoshiriki fainali za Afcon mwaka huu, wanatarajiwa kuwasili kambini kuanzia kesho Jumapili baada ya kutakiwa kufanya hivyo ili kuungana na wenzao wakati makocha nao wakirejea kutoka mapumzikoni.

Beki Mkongomani Henock Inonga ndiye mchezaji pekee ambaye atakosekana kutokana na kusalia kwenye kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo kilichotinga hatua ya 16 bora ya Afcon msimu huu.

Kocha Mkuu wa chama hilo, Mualgeria Abdelhack Benchikha, msaidizi wake Farid Zemiti na kocha wa Utimamu wa Mwili (fitness), Kamal Boudjenane wanatarajia kuanza kazi Jumatatu baada ya kuwasili kutoka mapumzikoni nchini kwao na sasa kikosi kipo chini ya Selemani Matola.

Mchezo ujao wa mashindano kwa Simba utakuwa Februari 17, mwaka huu itakapocheza na Dodoma Jiji katika Ligi Kuu, lakini gazeti hili linajua kabla ya hapo kikosi hicho kitatesti mitambo kwa kucheza mechi mbili za kirafiki na timu za madaraja ya kati kutoka Dar es Salaam.

Simba ipo nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu Bara ikiwa na alama 23 baada ya mechi 10, pia ipo hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na inashiriki Kombe la Shirikisho (ASF

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO....NABI AOMBA SIKU 30 TU ZA KUFANYA KAZI YA KUITIKISA AFRIKA....ALIA NA MUDA...