Home Habari za michezo FT: SIMBA 4-0 TEMBO FC….KARABAKA, JOBE WAANZA NA GIA KUBWA KWA BENCHIKHA…

FT: SIMBA 4-0 TEMBO FC….KARABAKA, JOBE WAANZA NA GIA KUBWA KWA BENCHIKHA…

Habari za Simba leo

SIMBA imetinga hatua ya 32 bora kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la (ASFC) na kuifuata Yanga baada ya kuitoa Tembo SC kwa mabao 4-0 Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Mabao yote yamefungwa na Luis Miquissone dakika ya 11 akipokea pasi kutoka kwa Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na la pili likifungwa na Saidi Ntibazonkiza dakika ya 31 kwa kichwa.

Mengine yalifungwa na Salehe Karabaka na Pa Omar Jobe wote wakiingia kipindi cha pili.

Mabadiliko aliyofanya Kocha Abdelhak Benchikha yalionekana kumlipa baada ya kuwatoa wachezaji wawili Balua nafasi yake ikichukuliwa na Jobe na kumtoa Fred Michael nafasi yake ikichukuliwa na Karabaka.

Kipindi cha kwanza Simba ilimiliki mpira ikisogea langoni mwa Tembo lakini kukosa utulivu kwa wachezaji wawili, Balua na Fred kuliinyima nafasi Simba ya kupata mabao mengi na kuifanya iende mapumziko kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili Tembo nayo ilibadilika na kuipa wakati mgumu Simba kulifikia lengo lao kwani hadi dakika 30 haikuruhusu bao.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Simba kuifuata Yanga iliyoitoa Hausung FC kwa mabao 5-1 Uwanjani hapo.

Kikosi cha leo : golini Hussein Abel, Hussein Kazi na Kennedy Juma, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na Israel Mwenda, Edwin Balua na Luis Miquissone, Shomari Kapombe, Sadio Kanoute, Saido Ntibazonkiza na Fredy Michael.

SOMA NA HII  RASMI..JAMES KOTEI KUKIPIGA CHAMAZI COMPLEX...ISHU NZIMA IKO HIVI AISEE....