Home Habari za michezo HII NDIO JEURI YA YANGA YA ENG HERSI HUKO MISRI….WAFIKIA HOTELI YA...

HII NDIO JEURI YA YANGA YA ENG HERSI HUKO MISRI….WAFIKIA HOTELI YA KISHUA..AL AHLY WAOGOPA…

Habari za Yanga leo

Yanga tayari ipo jijini Cairo, Misri kwa ajili ya pambano la mwisho la Kundi D katika Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly, huku mabosi wa klabu hiyo wakiificha timu katika kambi ya kishua ili kuwafanya wachezaji wasiwe na stresi na kuendelea kuwapa raha mashabiki wanaosubiri kuona timu ikiwatoa nishai wenyeji wao.

Kambi hiyo ya Yanga ipo umbali wa dakika 15 kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cairo ambako msafara wa wawakilishi hao wa Tanzania ukiwa na watu 60 ulitua na moja kwa moja kwenda hoteli ya nyota tano ya Royal Maxim Palace Kempinski kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa Ijumaa, Machi Mosi.

Yanga inavimba tu huko nje ya Tanzania kwa kufikia katika hoteli yenye hadhi ya maana huku ikiwa tayari na tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo baada ya wikiendi iliyopita kuwaadabisha CR Belouizdad kwa kuwachapa mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Benjamani Mkapa.

Unaambiwa gharama ya kulala usiku mmoja kwenye hoteli hiyo ya kishua kwa mtu mmoja ni Dola 305.43 ambazo ni zaidi ya Sh778,849 na kwa msafara wa watu 60 ukiondoa punguzo ambazo klabu zimekuwa zikipewa kwa siku mbili za kuwa huko ni mamilioni ya hela yamewatoka na bado gharama za usafiri.

Kila chumba kwenye hoteli hiyo kina runinga, lakini eneo ambalo watu wanaweza kukaa na kupiga stori, pia kuna bafu kubwa na la kisasa ambalo hupoza na kupasha maji moto kwa namna unayotaka.

Inaelezwa wageni wanaweza kufurahia aina mbalimbali za mapishi na starehe katika mojawapo ya migahawa mikubwa na baa tisa zilizopo hoteni hapo. Yapo mabwawa makubwa na ya kisasa ambayo wachezaji wa Yanga wanaweza kuogelea na kucheza michezo mbalimbali ya kujenga umoja kwenye timu.

Hoteli nyingine za hadhi ya Royal Maxim Palace Kempinski ambazo Yanga ingeweza kufikia mbali ya hiyo ni pamoja na Hilton Cairo Heliopolis, Four Seasons Hotel Cairo, Holiday Inn & Suites Cairo Maadi, Inter Continental Citystars Cairo, IHG Hotel na Sofitel Cairo Nile El Gezirah.

Kitendo cha Yanga kufikia katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano kinaweza kuwajenga wachezaji kuwa na utulivu kimchezo utakaoamua nani awe kinara wa Kundi D, kwani watetezi wa taji hilo Al Ahly kwa sasa ndio wanaoongoza wakiwa na pointi tisa wakati Yanga inazo nane.

Ushindi kwa Yanga utaifanya ifikishe alama 11 na kuiengua Al Ahly, lakini kama mechi itaisha kwa sare yoyote itakuwa na maana wenyeji watamaliza kama vinara wa kundi na Yanga kushika nafasi ya pili, ikisaliwa na pointi nane zinazoweza kufikiwa na CR Belouizdad itakayoikaribisha Medeama ya Ghana kwenye mechi nyingine ya kundi hilo.

Hata kama CR Belouizdad itashinda itafikisha pointi nane kama za Yanga, kwani kwa sasa ina pointi tano, lakini matokeo ya jumla baina yao yanaiengua kuipiku Yanga na kama itachapwa itamaliza ikiwa mkiani, kwani Medeama yenye pointi nne itafikisha saba,licha ya kwamba zote zimeshaaga michuano mapema.

SOMA NA HII  CHAMA,MUSONDA WAREJEA ZAMBIA..... ISHU IKO HIVI