Home Habari za michezo KUELEKEA AFCON 2023:- TAIFA STARS WAAPA ‘KUFA’ NA MOROCCO MECHI YA UFUNGUZI….

KUELEKEA AFCON 2023:- TAIFA STARS WAAPA ‘KUFA’ NA MOROCCO MECHI YA UFUNGUZI….

Habari za Michezo leo

KOCHA Msaidizi wa timu ya Taifa Stars, Hemed Morocco amesema mkakati wao kuanza vema michuano ya mataifa ya Afrika kwa kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa kwanza wa makundi ya fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Morocco utakaochezwa Uwanja wa San Pedro, Ivory Coast, Januari 17.

Kikosi cha Stars kipo katika mji wa San Pedro nchini Ivory, kwa ajili ya mashindano ya AFCON yanayotarajiwa kuanza kesho ( Januari 13) hadi Februari 11, mwaka huu Tanzania itatupa karata yao ya kwanza kwa kumenyana na Morocco, DR Congo na Zambia katika kundi F.

Kocha Morocco amesema hali ya hewa ni nzuri haitaathirika program za maandalizi ya michuano hiyo na wamesahihisha makosa yaliyojitokeza kwenye mechi ya kirafiki na wanaendelea kujinoa kwa ajili ya kukabiliana dhidi ya Morocco.

Amesema tayari wameweja sawa mipango mkakati kuelekea mchezo huo wa kwanza dhidi ya Morocco ambao utakuwa na ushindani kwa sababu ya hivi karibuni walicheza nao katika michuano ya kuwania kufuzu kombe la Dunia na kupoteza kwa kufungwa bao 2-0.

“Tumefanya kazi kwenye mapungufu ya kikosi chetu na utakuwa mchezo wa ushindani mkubwa sana kwa sababu Morocco tumeshawahi kucheza nao hivi karibuni, kila mmoja anamfahamua mwenzake lakini tumeandaa kikosi na wachezaji wako tayari kwa mapambano ya michuano hiyo,” Amesema Morocco.

Naye beki wa kati wa Stars, Dickso Job Amesema wamefanya mazoezi na wako tayari kwa michuano hiyo na wanaangalia kwanza mechi iliyopo mbele yao dhidi ya Morocco ambao utawapa dira la wapi wanaelekea katika michuano hiyo.

Amesema wanaifahamu vizuri Morocco kwa sababu tuliwa kucheza nao, wamejiandaa kwa mpango mkakati kuhakikisha wanafanikiwa kufanya vizuri na kuhakikisha wanavuka katika hatua ya makundi na kusonga mbele.

“Kwa sasa cha muhimu ni dhidi ya Morocco, tuko tayari kupambana na mechi yetu hiyo pamoja na michuano yote kuhakikisha tunaipeperusha vema bendera ya Tanzania, ninaimani tukipambana na kujitoa kwa asilimia 100 tunavuka kwenye makundi,” amesema Job.

Ameongeza kuwa kundi ngumu kulingana na kila timu imejiandaa vizuri kwa sababu ya wachezaji wazuri na na kila timu imejiandaa kwa ajili ya michuano hiyo na anaimani wanaenda kushindana na wapinzani wao, akiwemo Morocco, DR Congo na Zambia.

SOMA NA HII  BAADA YA OKRAH...ANAYEFUATIA KUTAMBULISHWA YANGA NI HUYU HAPA...JAMAA ANAJUA MNOO..