Home Habari za michezo PACOME APELEKEWA AL AHLY….GAMONDI AANZA KUFANYA YAKE…

PACOME APELEKEWA AL AHLY….GAMONDI AANZA KUFANYA YAKE…

Habari za Yanga leo

Kiungo kutoka nchini Ivory Coast Pacome Zouzoua aliyewatesa Waarabu wa Misri, Al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kaongezewa dozi ndani ya kikosi hicho chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Pacome ni mtambo wa mabao ndani ya Young Africans katika mashindano ya CAF akiwa katupia mabao matatu miongoni mwa timu alizozitungua ni Al Ahly kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Bao hilo lilichaguliwa kuwa bao bora alilifunga akiwa katikati ya mabeki watatu wa Al Ahly ambao walikwama kumzuia, hata Medeama FC ya Ghana aliwafunga mabao ya mtindo huo nje ndani.

Gamondi ameweka wazi kuwa ni muhimu wachezaji wote kuwa na mwendelezo mzuri kwenye uwanja wa mazoezi ili kuwa bora kila wakati kwenye mechi za ushindani.

“Wachezaji wote ni muhimu kufanya kazi kubwa uwanjani kwa ajili ya kuwa imara kwenye mechi za kitaifa na kimataifa kazi ni kubwa na muhimu kujituma.

“Kila mmoja ana nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi ambazo tunacheza iwe ni Khalid Aucho, Pacome kikubwa ni kufanya mazoezi na kuna program ambazo huwa tunazifanya kwa ajili ya kuwa bora zaidi.”

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKITAMBA NA BEKI WAO MCAMEROON...YANGA WAMESHUSHA CHUMA HIKI CHA KAZI...