Home Habari za michezo HUU HAPA UKWELI SABABU YA MECHI YA SIMBA vs MTIBWA KUGHAIRISHWA MAPEMA….

HUU HAPA UKWELI SABABU YA MECHI YA SIMBA vs MTIBWA KUGHAIRISHWA MAPEMA….

Habari za Simba leo

MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro unatarajiwa kupangiwa tarehe mpya baada ya kupanguliwa kutokana na maandalizi ya mechi za kimataifa.

Klabu ya Simba chini ya Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi 15 imekusanya pointi 36 ikiwa nafasi ya pili.

Mchezo wake wa 15 ulichezwa dhidi ya JKT Tanzania na Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 na mfungaji alikuwa ni Clatous Chama.

Taarifa ambayo imetolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imeeleza kuwa kuahirisha mchezo kati ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar uliopangwa kuchezwa Februari 18, 2024 Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa ya TPLB, sababu za kuahirishwa kwa mchezo huo ni kutoa fursa kwa Simba SC, kujiandaa na safari yake ya kwenda Ivory Coast kusaka ushindi mchezo dhidi ya ASEC Mimosas kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Mchezo huo wa hatua ya makundi unatarajiwa kuchezwa Februari 23, 2024 ambapo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO....AZAM WALISUKUMA FUPA LA YANGA KWA FEI TOTO....

2 COMMENTS

  1. “Kughairishwa” maana yake nini? Acheni ujinga wa kubuni na kutumia maneno ambayo hayamo kwenye kamusi ya lugha ya taifa. Mmerukia kazi ambazo si zenu au hamziwezi. Rudi shuleni.

  2. Habari ndugu Masala, neno lilotumika ni sahihi kwa kuzingatia matamshi na lugha ya kiswahili, tafadhali kama una neno lingine, au usahihi wa neno hilo tuandikie hapa nasi tutazingatia.

    Shukrani.