Home Habari za michezo KUHUSU KUTUPIA SANA SAFARI HII…MUDATHIR AFUNGUKA A-Z ALIVYOPIKWA NA GAMONDI…

KUHUSU KUTUPIA SANA SAFARI HII…MUDATHIR AFUNGUKA A-Z ALIVYOPIKWA NA GAMONDI…

Habari za Yanga leo

KIUNGO wa Yanga, Mudathir Yahya amesema siri kubwa ya kufunga bao kwa msimu huu ni baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi kumuingezea majukumu ndani ya uwanja.

Amesema kulingana na majukumu hayo atafunga sana kwa sababu anatakiwa kukaba, kuchezesha na kazi kubwa kuhakikisha nashambulia kwa kufika katika boksi la mpinzani, katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mudathir amesema bao alizofunga sita kwa aina moja hiyo, ni kufuata maelekezo aliyopewa na kocha Gamondi, kumtaka uwanjani kufanya majukumu yake , kushambulia na kufika ndani ya 18 ya mpinzani wanapokuwa na mpira.

Amesema kuzuia pale wapinzani wanapokuwa na mpira kuhakikisha wahafiki katika eneo lao na kusababisha madhara jambo ambalo amekuwa analifanya sana msimu huu chini ya Gamondi.

“Tangu 2013 nimeanza soka msimu huu nafunga sana, hakuna siri yoyote zaidi kujitoa na kujituma na kufanyia kazi mipango ya kocha anataka nijiongeze kwenye boksi nafanya hivyo na kuweza kufunga.

Gamondi ananipa majukumu yote uwanjani, kukaba, kuchezesha na kushambulia kwa kufika ndani ya boksi, nitafunga sana , nimeamibiwa na yote kwa sababu ya uwezo wangu wa kucheza nafasi nyingi uwanjani,” amesema Mudathiri.

Ameongeza kuwa hataki kumuangusha kocha wake kwa sababu amemuamini na kumpa nafasi hali ambayo anajitoa na kupambana kuhakikisha anasaidia timu yake kuvuna pointi tatu muhimu katika michezo ya ligi kuu na Kimataifa.

Mudathir ameeleza kuwa anatarajia kuendelea kufunga katika michezo ya ligi hiyo kuhakikisha wanatetea taji lao la ubingwa na michezo ya hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa kwa kutafuta pointi tatu dhidi ya CR Belouizdad watakaocheza Februari 24, uwanja wa Benjamin Mkapa na Marchi 1, mwaka huu dhidi ya Al Ahly.

Kiungo huyo amefikisha idadi ya mabao sita ameweka rekodi ya kuwa mkali wa kutibua mipango na kusaidia timu yake kuipa pointi tatu katika michezo migumu na muhimu.

Ikumbukwe kwamba Yanga ilipata sare yake ya kwanza msimu wa 2023/23 Februari 2 ubao wa Uwanja wa Kaitaba uliposoma Kagera Sugar 0-0 Yanga ambapo wapinzani wao walitumia mbinu ya kujilinda zaidi.

Ngoma ilikuwa nzito Februari 5 baada ya dakika 85 za kucheza bila kufungwa, Dodoma Jiji walishuhudia bao la jioni likifungwa na Mudathir dakika ya 86 akitumia pasi ya Nickson Kibabage.

Ipo wazi kwamba wakali wote hao wawili walianzia benchi, Mudathir aliingia dakika ya 61 akichukua nafasi ya Jonas Mkude na Kibabage aliingia dakika ya 76 akichukua nafasi ya Joyce Lomalisa.

Mchezo mwingine uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na Mudathir kutibua mipango kwa bao la usiku ilikuwa dhidi ya Namungo, ilikuwa ni Septemba 20 2023 alipofunga bao dakika ya 87.

Bao hilo alilofunga kiungo huyo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo ilikuwa ni zama za Cedrick Kaze ndani ya Namungo FC.Februari 8 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 2-1 Mashujaa, bao la ushindi lilifungwa na Mudathir dakika ya 85 na alifunga tena juzi katika mchezo dhidi ya KMC FC.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUWA KWA SASA HATAJWI TAJWI SANA...MAKAMBO AZIDI KUKIMBIZA MWIZI KIMYA KIMYA...