Home Habari za michezo MBELEKO YA CAF YAIBEBA TAIFA STARS KUFUZU AFCON 2025 YA MOROCCO….’TUSHINDWE SIE’...

MBELEKO YA CAF YAIBEBA TAIFA STARS KUFUZU AFCON 2025 YA MOROCCO….’TUSHINDWE SIE’ TU…

Habari za Michezo leo

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeruka kihunzi cha kwanza katika ndoto ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2025 zitakazochezwa mwakani huko Morocco baada ya kupangwa kuanzia hatua ya makundi ya kuwania kufuzu fainali hizo.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ imeeleza kuwa ni timu nane ambazo zitaanzia hatua ya awali ya mashindano ya kuwania kufuzu AFCON 2025 mwakani huku nyingine 44 ikiwemo Taifa Stars zikianzia moja kwa moja hatua ya makundi.

Timu nane ambazo zimepangwa kuanza hatua ya awali kuwania kufuzu AFCON 2025 ni Somalia, Djibouti, Sao Tome, Chad, Mauritius, Sudan Kusini, Liberia na Eswatini.

Sababu ya timu hizo kuanzia hatua ya awali ni kuwepo katika nafasi nane za mwisho za viwango vya ubora wa soka Afrika kwa mujibu wa chati iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani ‘FIFA’ mwezi huu ambapo zitapangwa kukutana zenyewe kwa zenyewe kupata nne zitakazoungana na nyingine 44 ili kuwa 48 zitakazotengeneza makundi 12 yatakayotoa timu 24 zitakazofuzu.

Droo ya hatua hiyo ya awali ya kuwania kufuzu AFCON 2025, imechezeshwa jana Jumanne (Februari 20) Cairo, Misri kuanzia saa 8:00 mchana kwa muda wa Afrika Mashariki na mechi za hatua hiyo ya awali zitachezwa kati ya Machi 18 hadi 26 mwaka huu kwa mtindo wa mtoano wa mechi mbili za nyumbani na ugenini.

Akizungumzia suala hilo, mchezaji wa zamani wa Taifa Stars, Adolph Rishard amesema kuwa kitendo cha Taifa Stars kutoanzia hatua ya awali kina faida kubwa kwani mechi za mtoano hazitabiriki.

“Kwa sisi makocha hakuna mechi ambazo zimekuwa zikituumiza kichwa kama za mtoano ambazo mnacheza mbili tu kusaka nafasi moja kuingia hatua inayofuata, kwa sababu zinachezwa ndani ya muda mfupi, hivyo hazitoi muda wa kutosha wa kupumzika kwa wachezaji na kufanya programu za kurekebisha tofautina mechi za makundi,”

“Jambo muhimu ni kujiandaa mapema maana kwa kile kilichoonekana kwenye AFCON 2023, nadhani kila timu sasa inajipanga” amesema Adolf Rishard, nyota wa zamani wa Stars

SOMA NA HII  HII 'UNBEATEN' YA YANGA HAIKUJA HIVI HIVI....KARIBU BILIONI KUMI ZIMETUMIKA...UKWELI HUU HAPA...