Home Habari za michezo BAADA YA MASTAA WAPYA SIMBA KUANZA KUKIWASHA…MATOLA KAIBUKA NA HILI JIPYA…

BAADA YA MASTAA WAPYA SIMBA KUANZA KUKIWASHA…MATOLA KAIBUKA NA HILI JIPYA…

Habari za Simba leo

Mara baada ya Washambuliaji wapya wa Simba SC kuanza kwa moto kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports dhidi ya Tembo FC juzi Jumatano, Kocha Msaidizi wa Simba SC, Selemani Matola amechimba mkwara mzito kuwa bado Wanasimba hawajaona asilimia 100 ya mastaa hao na baada ya muda wataona balaa lao.

Juzi Jumatano (Januari 31) Simba sc walishuka kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuvaana na Tembo FC katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports na kuishuhudiua timu hiyo ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Katika mchezo huo kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha alianza na mastaa wawili wapya ambao ni mshambuliaji Muivory Coast, Michael Koublan na winga mzawa, Edwin Balua, huku baadae akiingia straika mwingine mpya, Pa Omar Jobe.

Koublan ambaye alitumika kwa dakika 45 tu, alifanikiwa kuhusika kwenye bao moja kwa kutoa asisti ya bao la Luis Miquissone, huku Jobe ambaye aliingia kipindi cha pili na yeye akifanikiwa kufunga bao kwa kutumia asisti ya Saido Ntibazonkiza.

Akizungumza kuhusu kiwango cha mastaa hao wapya ambao walicheza mchezo wao wa kwanza juzi Jumatano (Januari 31), Matola amesema: Tunashukuru Mungu kwa kufanikiwa kupata matokeo ya ushindi na kusonga mbele katika mashindano haya, licha ya udogo wa jina la wapinzani wetu lakini walikuwa washindani bora uwanjani.

Tumeanza na baadhi ya wachezaji wetu wapya ambao wamesajiliwa katika dirisha hili dogo kwa kuwa wamefanya vizuri mazoezini na kila mtu anaona wamechangamka, jambo la msingi ni tuwape muda kidogo, uwezo walioonyesha sio asilimia 100 ya wanachoweza kufanya, hivyo baada ya muda watakuwa bora zaidi na kufunga mabao mengi.”

SOMA NA HII  BENDERA YA TANZANIA YAZIDI KUPEPEA AFRIKA...TWIGA STARS WAANZA KUGAWA DOZI MASHINDANO MAKUBWA ...