Home Habari za michezo BACCA AFIKIWA YANGA….UJUMBE ALIOPEWA AKISHINDWA NI YEYE BINAFSI AISEEE…

BACCA AFIKIWA YANGA….UJUMBE ALIOPEWA AKISHINDWA NI YEYE BINAFSI AISEEE…

Habari za Yanga SC

Aliyekuwa nahodha Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ ana kazi ya kulinda kiwango chake, kitakachofanya jina lake liendelee kuwa na heshima mbele ya mashabiki.

Cannavaro ambaye kwa sasa anaishi Marekani, alikiri kiwango cha Bacca kipo juu, pamoja na hilo alimtaka awe na tahadhari ya kuangalia mambo ya uwanjani zaidi yasije yakayumbishwa na umarufu alionao.

Ndani ya misimu 12 aliyocheza Yanga, Cannavaro aliyecheza kwa kiwango cha juu, hivyo anatamani Bacca afanye makubwa zaidi yake.

“Bila nidhamu mchezaji hata kama ana kipaji kiasi gani,inakuwa ngumu kufanya mambo makubwa, umaarufu una mambo mengi,ndio maana namshauri Bacca aangalie zaidi uwanjani,”alisema na kuongeza;

“Bacca naamini akiwa na muendelezo na kiwango chake, anaweza akafika mbali zaidi, japokuwa siyo muda wote naweza nikafuatilia kila kitu, ila anajua kukaba na kuziona hatari kwa haraka zaidi.”

MATAJI

Cannavaro aliisaidia Yanga kunyakua mataji ya Ligi Kuu manane 2006, 2007, 2009, 2011,2013,2015, 2016 na 2017, Wakati Ngao ya Jamii manne,2010,2013, 2014 na 2015.

Kagame Cup mataji mawili 2011 na 2012 na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) moja 2016/17. BACCA Bacca ambaye alijiunga na Yanga mwaka 2022 akitokea KMKM, aliisaidia timu hiyo kunyakua taji moja la Ligi Kuu, Ngao ya Jamii moja na la Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) (2022/23), hivyo bado ana safari ndefu ya kuifanyia makubwa klabu hiyo.

SOMA NA HII  TETESI: DJUMA WA AS VITA ASAINI MIAKA MIWILI YANGA...