Home Habari za michezo INONGA NA SIMBA NDIO BASI TENA….AMALIZANA NA TIMU YA NABI KIMYA KIMYA….KUONDOKA...

INONGA NA SIMBA NDIO BASI TENA….AMALIZANA NA TIMU YA NABI KIMYA KIMYA….KUONDOKA BUREE..

Habari za Simba leo

Kwa kiswahili cha kijiweni wanasema; “Imeisha.” Beki kitasa cha Simba aliyeng’ara na DR Congo kwenye Afcon, amefanya uamuzi wake kimyakimya na akapiga kimya vilevile.

Na uamuzi huo unamaanisha kwamba atakuwa ndani ya jezi ya Simba katika mechi zisizozidi 15 tu za mzunguko wa pili wa ligi, baada ya hapo ndiyo hivyo tena.
.
Habari za uhakika kabisa kutoka kwenye vyanzo ni kwamba staa huyo ambaye mkataba wake na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu, amesaini mkataba wa awali na FAR Rabat inayoongoza Ligi Morocco.

Kumbuka hii ndiyo timu anayoichezea Bernard Morrison ikifundishwa na Kocha wa zamani wa Yanga, Nabi Mohammed. Inonga tayari amerejea nchini akitokea kwao DR Congo baada ya kuiwezesha nchi yake kuwa mshindi wa nne katika AFCON.

Taarifa kutoka nchini Morocco ni kwamba Inonga ameingia makubaliano ya awali na klabu ya FAR Rabat ambayo yatamfanya mwisho wa msimu kwenda kusaini mkataba wa miaka mitatu na vinara hao wa Ligi ya nchini humo maarufu kama Botola.

SOMA NA HII  DUNDA NA MSHIKO KUTOKA SLOT YA LAS VEGAS KUPITIA UFALME WA MERIDIANBET...

2 COMMENTS

  1. Kwa hiyo ule mkataba aliongeza mwaka Jana ulikua feki Eti hii ndio bongo mpaka waandishi Ni waongo ambao habari zenu zinasomwa na kila mtu