Home Habari za michezo KUHUSU UFUNGAJI BORA…MPAKA SASA AZIZ KI KAMPIGA ‘KABALI YA KOO’ SAIDOO…KANUNI HIZI...

KUHUSU UFUNGAJI BORA…MPAKA SASA AZIZ KI KAMPIGA ‘KABALI YA KOO’ SAIDOO…KANUNI HIZI HAPA…

Habari za Michezo leo

Nyota wa Yanga, Stephane Aziz KI amejikusanyia jumla ya pointi zake 19 katika Ligi Kuu Bara msimu huu na kumpiku kiungo mshambuliaji wa Simba Mrundi, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ mwenye pointi sita akiwa na kikosi hicho cha Msimbazi.

Iko hivi! Aziz KI ndiye kinara wa ufungaji hadi sasa msimu huu akifunga mabao 10, nyuma ya nyota wa zamani wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliyeko Azam FC mwenye manane huku kwa upande wa Saido aliyekuwa katika kiwango kizuri akiwa amefunga matano.

Kwa mujibu wa kanuni mpya ya Ligi Kuu Bara msimu huu, Aziz KI anapata pointi 19 kutokana na mabao 10 aliyofunga ambapo tisa kati yake ameyafunga kawaida huku moja pekee akifunga kwa mkwaju wa penalti tofauti na ilivyo kwa upande wa Saido ambaye ana mengi ya penalti.

Msimu uliopita kulikuwa na malalamiko mengi baada ya Saido kufungana na Fiston Mayele kwenye chati ya ufungaji kila mmoja akifunga 17, lakini mashabiki wengi walilalamika wakiamini kuwa Mayele anastahili tuzo hiyo peke yake kwa kuwa alikuwa na mabao machache ya penalti tofauti na Saido, hali ambayo ililazimisha kanuni ya tuzo ya ufungaji kubadilishwa.

Kanuni ya (13.1) ya Ligi Kuu Bara kuhusu tuzo ya mfungaji bora inasema mabao yatakayofungwa kwa njia ya kawaida yatakuwa na pointi mbili (2), huku yatakayofungwa kwa mkwaju wa penalti yatapewa pointi moja (1) hivyo mwenye alama nyingi atakuwa mshindi.

Kama itatokea watalingana basi itatumika kanuni ya 13.2, ambayo itatoa nafasi kwa aliyecheza muda mchache zaidi kuibuka mshindi na ikishindikana tena kwa vigezo hivyo itatumika kanuni ya 13.3 ya mchezaji aliyefunga mabao mengi ugenini.

Katika mabao 10 aliyofunga Aziz Ki moja ni la mkwaju wa penalti kati ya mawili aliyofunga kwenye ushindi wa mabao 4-1, dhidi ya Mtibwa Sugar Desemba 16, mwaka jana huku mengine yakifungwa na Kennedy Musonda na Mahlatse Makudubela ‘Skudu’.

Kwa upande wa Saido, katika mabao yake matano aliyoyafunga msimu huu tayari manne ni ya penalti huku moja pekee akifunga kawaida.

Mabao ya penalti aliyofunga Saido amezifunga timu za Tanzania Prisons, Kagera Sugar, KMC na Mashujaa huku mchezo pekee aliofunga bao la kawaida ni ule wa Singida Fountain Gate uliopigwa Oktoba 8, mwaka jana na Simba kushinda kwa mabao 2-1.

Aliyekuwa mchezaji wa Simba mshambuliaji, Jean Baleke aliyejiunga na Al-Ittihad ya Libya ndiye aliyekuwa anamkaribia Aziz KI kwani hadi anaondoka alikuwa amefunga mabao manane ya Ligi Kuu Bara huku moja tu akifunga kwa mkwaju wa penalti.

Bao alilofunga Baleke kwa mkwaju wa penalti ni katika ushindi wa mabao 3-0, dhidi ya Coastal Union Septemba 21, mwaka jana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam huku nyota huyo akiibuka shujaa wa mchezo baada ya kufunga yote matatu ‘hat-trick’.

Kwa maana hiyo Baleke licha ya kuondoka ila hadi sasa amejikusanyia jumla ya pointi 15 ambazo ni nyingi zaidi ya Saido.

Simba ambayo inacheza mchezo wake wa Ligi Kuu Bara wa 12 kesho, ipo nafasi ya tatu kwenye ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 26 lakini ikiwa imefunga mabao 24

SOMA NA HII  KUDADEKI....HII NDIO YANGA YA GSM...WACHEZAJI WAFANYIWA 'KUFRU' YA FUNGA MWAKA..SIMBA CHA MTOTO....