Home Habari za michezo KISA 6G YA JANA…KOCHA JWANENG AVUNJA UKIMYA….MASTAA SIMBA WAOGA MIL 500 ZA...

KISA 6G YA JANA…KOCHA JWANENG AVUNJA UKIMYA….MASTAA SIMBA WAOGA MIL 500 ZA USHINDI…

Habari za Simba leo

KOCHA Mkuu, Abdelhak Benchikha amesema wachezaji wake sasa wanaelekea kule kwenye Simba anayoihitaji, huku akiwa na imani wachezaji wake wanaweza kuonyesha kiwango huko mbele ya safari zaidi ya walichokionyesha katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Amesema katika mechi hiyo, wachezaji wameonyesha jinsi ya kupambana na kujituma na amewapongeza kwa kufanya kile ambacho amewatuma katika uwanjani na kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Simba alitinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kulipa kisasi kwa mpinzani wake Jwaneng Galaxy ya Botswana kwa idadi ya mabao 6-0 uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Baada ya kukamilika kwa mchezo huo wachezaji wa Simba wamefanikiwa kuvuna kiasi cha Million 530 ikiwa ni fedha za bonasi kutoka ndani ya klabu hiyo na kapu la mama ambalo linatolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan

Rais Samia Suluhu Hassan ametupongeza kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichakaza bila huruma Jwaneng Galaxy kutoka Botswana kwa mabao 6-0 na kusema ushindi huo sio tu kwa ajili ya Simba pekee bali ni Watanzania wote.

“Hongereni sana Klabu ya Simba kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mafanikio yenu sio furaha na fahari kwa mashabiki na wanachama wa Simba bali pia kwa Taifa na Watanzania wote,” amesema Rais Dkt. Samia.

Benchikha amesema nawapongeza wachezaji na mashabaki, wamecheza mchezo mzuri kiufundi kwa kufunga bao 6.

Amesema anafuraha sana kwa wachezaji wake kuonyesha moyo wa kupambana anaimani ya kuendelea kufanya vizuri katika mashindano hayo hatua ya robo fainali.

“Niwapongeze wachezaji wamepambana sana, mashabiki kujitokeza kwa kusapoti timu yao , tulifanya maandalizi mazuri kwa kuzingatia mambo muhimu mbinu, ufundi, kisaikolojia kwa vijana wangu na kuwasisitiza katika kupambana

Wamefanya kile nilichowapa katika uwanja wa mazoezi kwa kushinda idadi kubwa ya mabao 6-0, kwangu tungeshinda bao 1-0 ingekuwa vizuri kwa kuwa tulihitaji kufuzu hatua nyingine,” amesema Benchikha.

Kuhusu kiwango cha kiungo wake, Clatous Chama, Kocha huyo amesema anaimani na uwezo wa nyota huyo ni mzuri hasa anapokuwa katika eneo la mpinzani.

“Ni mchezaji mzuri anakupa matokeo ukuangalia katika mchezo huu, ametoa pasi na amefunga bao, tumekosa nafasi nyingi tulitengeneza ikiwemo mbili kutoka kwake,” amesema Kocha huyo.

Ameeleza kuwa baada ya mechi hiyo wanaenda kujipanga kwa ajili ya mechi zilizopo mbele yao ikiwemo za Ligi Kuu Tanzania kabla ya kufanya maandalizi ya kujiandaa na michezo ya hatua ya robo fainali.

Naye kiungo wa Simba, Chama amesema furaha yake siku kutoa pasi wala kufunga bao bali ni kuona Simba inashinda kwa kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo.

Amesema anaimani haukuwa mchezo rahisi kwa kuwa walihitaji kupata ushindi ili kutinga hatua ya robo na wamefanikiwa hilo kwa kuwapa furaha mashabiki wanaosapoti timu.

“Ni ushindi muhimu sana kwangu, timu ikishinda ni furaha sana kwa sababu tumewafanya mashabiki wetu wanaotusapoti kuwa na furaha, kwangu kufunga au kutoa pasi sio jambo la kujivunia bali timu kushinda kwangu muhimu.

Huu ni ushindi mkubwa na mzuri, hii ndio Simba inayohitaji jambo lake tumeingia hatua ya robo sasa tunajipanga kwa hatua nyingine, Simba hii weka mbali na watoto,” amesema kiungo huyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah ‘Try Again’ amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa milioni 30 za ‘bao la Mama’ kufuatia ushindi wa mabao 6-0 tuliopata dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Pesa hizo zimekabidhiwa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro na kupokelewa na Try Again, Mwenyekiti wa Klabu Murtaza Mungungu na nahodha wa kikosi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.

Try Again amesema zawada inatoa hamasa kwa wachezaji kupambana kwa ajili ya timu na mwisho wa siku mafanikio ya kwa timu na Taifa kwa ujumla.

“Tunamshukuru Rais Samia kwa zawadi hii, baada ya kuipata hii tunaenda kujipanga kwa ajili ya robo fainali na mipango yetu ya kuvuka zaidi, mbali na pesa hizo pia wamekabidhi Million 100 kutoka kwa Rais wa Heshima wa Simba, Mohammed Dewji na klabu itatoa mill 400 kama ahadi yao,” amesema Try Again.

Amesema anawapongeza wachezaji, benchi la ufundi na kuwashukuru mashabiki kujitokeza kwa wingi kusapoti timu yao anaimani umoja na ushirikiano waliounyesha katika mechi na Jwaneng Gallaxy watafikia malengo yao kucheza nusu fainali.

“Mpira wa miguu unachezwa hadharani na sio mdomoni, tunaenda kujipanga na robo fainali ninaimani kwa umoja tulikuwa nao na kuendelea kushikamana na kuombea timu yetu na kutosikiliza maneno ambayo yatavunja umoja wao na kutaka kuvurugana,” amesema Try Again.

Kuhusu suala la kumuongezea mkataba Chama, Try Again amesema hilo ni jambo la pande mbili klabu na mchezaji, kwa sasa wanaangalia zaidi hatua iliyopo mbele yao kujipanga kwa ajili ya kucheza robo fainali.

“Niwapongeze wachezaji wote wamecheza vizuri sio Chama pekee aliyecheza uwanjani, mchezaji mzuri bado ni mali ya Simba,” amesema Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Wakurugenzi Simba.

Kocha wa Jwaneng Galaxy, Morena Ramoreboli amesema nawapongeza Simba kwa mchezo mzuri na kutengeneza mashambulizi mengi na kufanikiwa kushinda mabao 6-0.

Amesema wamepata wakati mgumu kuwazuia Simba ambao walifanya mashambulizi kupitia wachezaji watano, akiwa Kapombe (Shomari), Babacar Sarr, Said Ntibazonkiza, Chama, Fabrice Ngoma na Kibu Denis.

“Kipindi cha pili walifanya mabadiliko ambapo walimuingiza namba 34 (Ladeki Chasambi) walicheza kwa kasi na kufanikiwa kutufunga bao 3 zingine, jumla kuwa mabao 6-0, nimebeba makosa na kupata funzo kupitia mchezo huu na kujipanga kwa muda mwingine ,” amesema Morena

SOMA NA HII  KUELEKEA KESHO SIKU YA WANANCHI....PITSO MOSIMANE AIPA UJIKO YANGA...AAMUA KUPUMZIKA SOKA...