Home Habari za michezo MABILIONI YA CAF ‘YAPIGWA PANGA’ SIMBA, YANGA….MASTAA KUAMBULIA MGAO HUU….ISHU HII HAPA…

MABILIONI YA CAF ‘YAPIGWA PANGA’ SIMBA, YANGA….MASTAA KUAMBULIA MGAO HUU….ISHU HII HAPA…

Habari za Michezo leo

Kitendo cha miamba ya soka la Tanzania, Simba na Yanga kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kimezifanya timu hizo kuogelea minoti kutoka kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Rais Samia Suluhu Hassan, matajiri na wadau mbalimbali.

Kwa mujibu wa orodha ya viwango vya fedha kama zawadi ambazo CAF hutoa kulingana na hatua ambayo timu imefikia kwenye michuano hiyo ya kimataifa, Simba na Yanga kila mmoja itavuna Dola 900,000 (zaidi ya Sh2.2 bilioni sawa na Bil 4.8 kwa klabu zote) kutokana na kufika robo fainali.

Mkwanja ambao CAF imekuwa ikiutoa kwenye michuano hiyo ya kimataifa ambayo hufanyika kila msimu unalenga kuongeza ushindani kwa timu shiriki na pia kusaidia katika gharama ambazo zimekuwa zikitumia.

Rais Samia ameendelea kuzifanya klabu hizo kongwe nchini kuogelea minoti kwa msimu wa pili mfululizo ikiwa ni sehemu ya kuchochea hamasa kwa wawakilishi hao wa nchi katika michuano hiyo ya kimataifa, ambayo zimekuwa zikiipeperusha vyema bendera ya nchi

Katika hamasa yake, mkuu huyo wa nchi amekuwa akitoa Sh5 milioni kwa kila bao kwenye mchezo ambao zimeibuka na ushindi kuanzia katika hatua ya makundi.

Simba na Yanga kila moja kwenye hatua ya makundi imeshinda michezo miwili, Mnyama akishinda dhidi ya Wydad Casablanca kwa mabao 2-0 na Jwaneng Galaxy F.C mabao 6-0, hivyo imejikusanyia Sh40 milioni ilhali upande wa Wananchi ni dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria mabao 4-0 na Medeama ya Ghana mabao 3-0, hivyo kutoka kwa Mama vijana wa kocha Miguel Gamondi wamevuna Sh35 milioni.

Kwa kile ambacho wawakilishi hao wa Tanzania walichofanya kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Mama amewapongeza na anaamini watani hao wa jadi wataendelea kufanya vizuri kwenye hatua ya robo fainali ambayo droo yake itachezeshwa Machi 13.

Kwa ujumla Simba imevuna jumla ya Sh500 milioni kama zawadi kwa kufuzu robo fainali achana na ule mkwanja wa CAF, ikiwemo Sh100 milioni ambazo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro alimkabidhi meneja wa timu hiyo, Mikael Igendia zilizotolewa na rais wa heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewji.

Mastaa wa Yanga nao wameogelea minoti ambayo ni zaidi ya Sh 400 milioni kutoka kwa mfadhili wao, Ghalib Said Mohamed pamoja na wadau wengine.

SOMA NA HII  ISHU YA 'SUB' YA CHAMA...MGUNDA NAYE ASHINDWA KUJIZUIA...AIBUKA NA HILI KUHUSU MBRAZILI...