Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI IJAYO YA LIGI….ZAHERA AWAPIGA MKWARA WA KUFA ‘NTU’ YANGA…

KUELEKEA MECHI IJAYO YA LIGI….ZAHERA AWAPIGA MKWARA WA KUFA ‘NTU’ YANGA…

Habari za Michezo

BAADA ya kupata ushindi wa kwanza baada ya siku 88 sawa na miezi mitatu, juzi Namungo FC iliichapa Kagera Sugar bao 1-0 na Kocha Mwinyi Zahera ameibuka na kuitisha Yanga, labda wasije.

Namungo itaikaribisha Yanga Ijumaa kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara na Zahera anaamini vijana wake baada ya ushindi dhidi ya Kagera, morali imeamka na hivyo mabingwa hao watetezi wa michuano hiyo wasitarajie ushindi.

Mara ya mwisho kwa Namungo kupata ushindi kwenye mechi za Ligi Kuu Bara ni mwaka jana Desemba 7 dhidi ya Mtibwa Sugar, ikishinda bao 1-0.

Kwenye mechi tano ilizocheza kabla ya ushindi wao na Kagera Sugar ilikubali vichapo viwili dhidi ya Mashujaa (1-0), Tanzania Prisons (1-0) huku ikiambulia sare tatu dhidi ya KMC (2-2), JKT Tanzania (0-0) na Tabora United (1-1).

Zahera amesema walikuwa na ratiba ngumu kwenye mechi zote tano na walikuwa ugenini, sasa wamerudi nyumbani na wao watahakikisha hawapotezi pointi wakianza na vijana hao wa Jangwani.

“Mechi zote tano tulikuwa ugenini, nawapongeza wachezaji wangu kwa kufanikiwa kukusanya pointi tatu kati ya mechi hizo sasa ni zamu ya nyumbani tumeanza na Kagera Sugar anayefuata ajiandae;

“Hatutakiwi kudondosha pointi tena, tunahitaji kujikwamua kwenye hatari ya kushuka daraja nafasi tuliyopo sio salama kutokana na namna tulivyo pishana pointi chache na walio chini yetu,” alisema.

Zahera amesema anawaheshimu wapinzani wake Yanga huku akikiri wana kikosi kizuri lakini ana imani kubwa na wachezaji wake watapata matokeo mazuri.

“Hatukuwa na matokeo mazuri kwenye michezo iliyopita haina maana hatukuwa tunaonyeha upinzani, kuzidiwa mbinu ndio sababu ya kupoteza, ukiangalia mchezo hadi mchezo kulikuwa na mabadiliko ya uchezaji.”

“Nina imani kubwa, baada ya kurekebisha makosa kwa kiasi kikubwa tumepata matokeo dhidi ya Kagera mchezo unaofuata ni dhidi ya Yanga waliotoka Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa bora na sisi tumejipanga kuonyesha mchezo mzuri na wa ushindani,” alisema.

SOMA NA HII  LAMINE AWEKWA MTU KATI YANGA KISA NIDHAMU