Habari za Yanga SC
Habari za michezo

GAMONDI:- HATA TUKIKUFANGA GOLI 5…TUTAENDELEA KUKUSHAMBULIA TU….

admin March 12, 2024 2:25 pm

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi amesema kuwa falsafa ya soka lake ni la kuburudisha hata kama itatokea anapoteza mchezo.

Gamondi ameingia kwenye vitabu vya Historia mpya ya Klabu ya Wananchi Yanga SC kwa kushinda bao 5 katika mechi nane ndani ya msimu wake wa kwanza tu kwenye timu hiyo.

“Ni bora unifunge kuliko nikuonyeshe udhaifu tena nyumbani kwangu, mimi mpira ni burudani nataka niburudishe halafu nishinde, ikitokea nimeshindwa basi nitakuwa nimeburudisha na ikitokea nimeshinda na kuburudisha pia.

“Siwezi kucheza na mabeki 9 halafu mshambuliaji mmoja hata kama naongoza kwa mabao matano nitaendelea kukushambulia tu,” amesema Kocha Miguel Gamondi.

◉ Yanga 5 – 0 KMC
◉ Yanga 5 – 0 JKT Tanzania
◉ Yanga 5 – 1 ASAS
◉ Yanga 5 – 1 Simba SC
◉ Yanga 5 – 0 Jamhuri
◉ Yanga 5 – 1 Hausing FC
◉ Yanga 5 – 0 Polisi Tanzania
◉ Yanga 5 – 0 Ihefu FC.

Mechi inayofuata ni Yanga dhidi ya Geita Gold FC.

Pengine Miguel Gamondi ndiye kocha katili zaidi kwenye historia ya Yanga SC?

ACHANA NA JACKPOT ZINGINE…HII HAPA BABA LAO YA EXPANSE STUDIO NDANI YA MERIDIANBET.. SHAFII DAUDA:- FEI TOTO WA AZAM NI BORA ZAIDI YA FEI TOTO WA YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply