Home Habari za michezo SKUDU:- KWA HAWA MAMELOD HAWA MHHHH….

SKUDU:- KWA HAWA MAMELOD HAWA MHHHH….

Habari za Yanga leo

Winga wa Klabu ya Yanga, Mahlatsi Makudubela ‘Skudu’ amesema kuwa anawafahamu vizuri miamba ya soka ya Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns ambao ni wapinzani wao kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya CAFCL, hivyo anao uhakika kuwa watashinda na kwenda nusu fainali.

Skudu ambaye amewahi kucheza timu kubwa za Afrika Kusini miaka ya nyuma ikiwemo Orlando, Chippa, Pretoria, Platinum, Mamelodi na Marumo na kabla ya kwenda kutua Yanga, amesema kwa kikosi cha Wananchi kilichopo sasa hivi, wanao uwezo mkubwa wa kupambana na Masandawana na kupata ushindi.

Droo ya robo fainali ya CAFCL imechezeshwa juzi ambapo Yanga imepangwa kucheza na Mamelodi huku Simba wao wakipangwa na Al Ahly ya Misri.

“Ni droo nzuri nay a kuvutia kwa klabu. Tumeingia kwenye robo fainali ya CAFCL kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi kupita, tusingeweza kujichagulia timu yoyote, tumejiandaa kwa timu yoyote itakayokuja mbele yetu. Tumepewa Mamwelodi Sundowns, ndicho kitu cha kwanza tunachokifikia vichwani mwetu kwa sasa.

“Tunapaswa kushinda mechi zetu dhidi ya Mamelodi. Hawa Mamelodi kwa kwa level ya Yanga na aina ya wachezaji tulio nao, tunaweza kula nao sahani moja. Tuna wachezaji wazuri wenye Kariba ya juu na uwezo mkubwa, tunaweza kwenda jino kwa jino na Mamelodi na tumejiandaa na tunataka kwenda nusu fainali.

“Kikubwa mashabiki zetu waendelee kutusapoti, wamekuwa na sisi tangu mwanzo, hivyo waendelee kutupa sapoti yao bila kujali nani yupo uwanjani nani hayupo, na sisi tutaoa kile tulichonacho kwa ajili. Yanga ni timu kubwa na yenye malengo makubwa, tunaamini tutafanya makubwa uwanjani.

“Yanga tuna mashabiki wengi sio Afrika Kusini tu bali Afrika nzima. Tulikwenda Rwanda kucheza na EL Merrikh tuliona mashabiki wengi wakitusapoti na kujaza uwanja.

“Tunaamini pale Afrika Kusini, uwanja utajazwa na Wananchi, kijani na njano ambayo hata Mamelodi wanaitumia. Sio kufia uwanjani tu bali tunaapa tutatoka jasho la damu uwanjani kuipambani Yanga yetu,” amesema Skudu.

SOMA NA HII  KUHUSU MAKUNDI KLABU BINGWA NA SHIRIKISHO CAF...SIMBA NA YANGA KUJUA MBIVU NA MBICHI TAREHE HII..