Home Habari za michezo AMBANGILE:- YANGA WAKIJISAHAU NA HILI WATAPIGWA GOLI ZA KUTOSHA NA MAMELOD….

AMBANGILE:- YANGA WAKIJISAHAU NA HILI WATAPIGWA GOLI ZA KUTOSHA NA MAMELOD….

Habari za Yanga leo

Kocha na mchambuzi wa boli, George Ambangile ameutaja udhaifu wa Yanga SC ambao amesema, mwalimu anatakiwa kuufanyia kazi kuelekea mechi yao dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Ambangile amesema, Yanga wanapokuwa na mpira wana udhaifu wa kuacha nafasi kubwa kutoka kwa mstari hadi mstari wa ukabaji jambo ambalo lina madhara makubwa kama mshindani.

“Hilo labda ndio wanapaswa Yanga kulifanyia kazi maana huwa wanaposhambulia, mabeki wao wa pembeni huwa wanakwenda mbele hivyo kuwaacha nyuma Job, Bacca na Aucho kama atakuwa fiti, ni rahisi sana kushambuliwa na kufungwa kama mtu akipitia katikati yao,” alisema Ambangile.

Yanga atawakaribisha Mamelodi Marchi 30, 2024 katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

MAMELOD KUTUA BONGO LEO.

Klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini itawasili Nchini Tanzania Siku ya Alhamis Maci 28, 2024.

Mamelodi watakuwa wageni wa Yanga Machi 30 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa mchezo wa Mkondo wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  GAMONDI AMKINGIA KIFUA HAFIZ KONKANI, ISHU IKO HIVI