Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba (CEO), Imani Kajula amesema kuwa timu hiyo imefanya usajili mkubwa hivyo wana uhakika watavuka kwenda nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Kajula amesema hayo wakati akifanya mahojiano na kituo cha Radio cha EFMÂ kuelekea mchezo wao wa robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya miamba wa Afrika Al Ahly ya Misri utakaopigwa kesho Ijumaa, Machi 29, 2024 katika Dimba la Mkapa.
Ikumbukwe kuwa, katika dirisha dogo, Simba imewasajili kiungo Babacarr Sarr, washambuliji fredy Michael na Pa Omar Jobe huku ikifanya usajili wa wachezaji watatu wa ndani ambao ni Ladack Chasambi, Edwin Balua na Saleh Karabaka.
“Tumefanya usajili bora na kwa umakini mkubwa msimu huu ambao utatusaidia kufika nusu fainali CAF Champions League”
“Tunamshukuru sana Mo Dewji. Ukiondoa pesa anayotoa kwa mwaka, lakini anatoa pesa nyingi za ziada. Mfano katika mchezo wa Jwaneng Galaxy alitoa bonasi ya Tsh milioni 100 kama hamasa ya mchezo.”
“Kuendesha timu kama Simba ni gharama kubwa sana, bajeti tu ya safari ya kutoka Tanzania kwenda kucheza Misri gharama inafika zaidi ya MILIONI 300,” amesema Imani Kajula.