Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO NA AL AHLY…CEO SIMBA AWEKA SILAHA HIZI HADHARANI…

KUELEKEA MECHI YA KESHO NA AL AHLY…CEO SIMBA AWEKA SILAHA HIZI HADHARANI…

Habari za Simba SC

UONGOZI wa Simba umesema wameandaa Silaha mbili zitakazowasaidia timu yao kufikia malengo yao ya kufanya vizuri katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri .

Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula aliweka wazi silaha hizo ni kutilia manani matakwa ya benchi la ufundi linaloongozwa na Abdelhak Benchikha pamoja na wachezaji, lakini na mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani.

Kesho Simba wanakibarua kigumu cha kusaka ushindi mnono katika mchezo huo dhidi ya Al Ahly katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam kabla ya kwenda kumaliza mchezo nchini Misri.

Mtendaji huyo amesema kwa misimu kadhaa Simba imekuwa ikiishia hatua ya robo fainali lakini wamefanya majaribio ya makusudi na mahususi kwa safari hii kwenda nusu fainali.

Amesema majaribo hayo ni kuandaa siraha hizo ikiwemo kumsikiliza Benchikha mahitaji yake ikiwemo kupata mazingira mazuri na kwenda Zanzibar kwa ajili maandalizi ya mchezo dhidi ya Al Ahly .

“Timu ilipokuwa Zanzibar tulipata mechi ya kirafiki ambayo imetupa maandalizi mazuri sana kocha imampa ufundi, kuona madhaifu ya kikosi chake pamoja na wale waliopo taifa Stars kurejea na kuungana na timu, Chama (Clatous) na wengine wamesharudi na kuungana na timu kambini.

Tunaiheshimu Al Ahly timu bora lakini tukumbuke tumekutana nao katika robo fainalo ya African Football League (AFL) na kutuondoa kikanuni, hakuna pasi na shaka kwamba kila mmoja wetu tunajua lakini tunahitaji kutumia uwanja wa nyumbani kutafuta ushindi mnono ambao tutawatoa wapinzani hapa nyumbani,” amesema Kajula.

Kuhusu viingilio, ameeleza kuwa wanawafahamu vizuri mashabiki hawana hofu juu ya ununuaji wa tiketi hali ambayo hawakutaka kuweka mechi hiyo bure hasa katika viti vya mzunguko.

“Tukumbuke ule uwanja sio bure unalipia na ukifanya bure basi unawanyima mapato Serikali, kwa sababu mzunguko unathamani ya asilimia 15 ya mapato ambayo ni nyingi kuliko viti vyote pale Benjamin mkapa

Silaha ya pili mashabiki tunatambua hawa ni wachezaji wa 12 uwanjani tunaimani nao kujitokeza wingi uwanjani kwa sababu mechi zote tulikuwa nao katika kila hatua,” amesema Kajula.

SOMA NA HII  JEAN AHOUA KUPEWA JEZI NAMBA 17...TAKWIMU ZAKE ZIKO HIVI.