Home Habari za michezo KUHUSU UBORA WA FREDY NA PA JOBE….UONGOZI SIMBA WAVUNJA UKIMYA…MSIMAMO HUU HAPA…

KUHUSU UBORA WA FREDY NA PA JOBE….UONGOZI SIMBA WAVUNJA UKIMYA…MSIMAMO HUU HAPA…

Habari za Simba leo

KLABU ya Simba imeweka wazi kuwa Moses Phiri bado ni mchezaji wa timu hiyo, mwenye mkataba wa mwaka mmoja zaidi na amepelekwa kwa mkopo katika klabu ya Power Dynamos ya Zambia.

Umesema hayo baada kuwa na maswali mengi juu ya kuachwa kwa mshambuliaji huyo aliyeondoka kipindi cha dirisha dogo akiwa na wastani mzuri wa kufumania nyavu huku nafasi zao wakiletwa Freddy Michael na Pa Omar Jobe.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula amesema Phiri ni mchezaji halali wa Simba, amepelekwa Power Dynamos kwa mkopo kwa ajili ya kurejesha ubora wake, na kama ikijiridhisha kuwa amerudi kwenye ubora wake unaofahamika, atarejea kwene mitaa ya Msimbazi..

Amesema hatua ya kupelekwa kwa mkopo Phiri ni baada ya kutokuwa kwenye ubora ambao alikuja nao na benchi la ufundi kupendekeza nyota huyo kupelekwa kwa mkopo.

β€œPhiri ni mchezaji wetu halali ana mkataba wa mwaka moja amepelekwa kwa mkopo klabu ya Power Dynamos ya Zambia kwa lengo la kupata nafasi ya kucheza na kurudi katika ubora wake,” amesema Kajula.

Ameongeza kuwa kutokana na kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza na baada ya kupona majeraha hakurejea katika kiwango chake hali iliyopeleka kumtoa kwa mkopo na kusajiliwa wengine.

Kajula amesema mbadala wa Phiri wameamua kuwasajili Freddy na Pa Jobe ambao wanatakiwa kupewa muda wa kuzoea mazingira kwa sababu usajili wa nyota hao umepitishwa na benchi la ufundi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSOTEA BENCHI SANA...YANGA WAAMUA KUACHANA NA 'NINJA' KWA STAILI HII MPYA...AKIZINGUA NDIO BASI TENA...