Home Habari za michezo BALAA LA NABI HUKO MOROCCO SIO POA…..WYADAD WAKIONA CHA MTEMA KUNI…

BALAA LA NABI HUKO MOROCCO SIO POA…..WYADAD WAKIONA CHA MTEMA KUNI…

Habari za Michezo leo

Kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi amejihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani timu yake ya FAR Rabat ikiongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Morocco (Botola Pro) na pointi 58, huku ikiitupa Wydad Casablaca nafasi ya tano na itakosa michuano hiyo mwakani.

Kocha huyo ambaye aliifikisha Yanga kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita na kushika nafasi ya pili, ameiongoza FAR Rabat katika mechi 24, ikifuatiwa na Raja Casablanca yenye pointi 54 na ina nafasi kubwa ya shiriki ligi hiyo sawa na FAR Rabat, huku RS Berkane nafasi ya tatu na pointi 40 ni kama imeshapotea njia.

Iko hivi. Nabi anahitaji mechi mbili tu kati ya sita zilizobaki kufikisha pointi 64, ambazo zitamhakikishia nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa, huku Raja nayo ikihitaji mechi tatu kufikisha 63, zikiiacha RS Berkane ambayo ikishinda michezo yote sita iliyobaki itafikisha pointi 62.

Ni wazi Presha kwa FAR Rabat na Raja haipo kapisa kwani kwenye mechi sita zilizobaki zina uhakika wa kushinda mechi hizo na ndio zilizo kwenye mbio za ubingwa na yoyote kati ya hizo ina nafasi ya kubeba msimu huu.

Nabi amekuwa na msimu mzuri na amefikisha pointi hizo 58 baada ya kushinda mechi 18, sare nne na kukubali vichapo viwili na endapo FAR itashinda michezo yote iliyobaki itafikisha pointi 79, huku Raja itafikisha 75 na hivyo zitatofautiana pointi nne.

Licha ya ubora ikwenye ligi kuu ya Morocco, Nabi ameshindwa kuifikisha mbali FAR Rabat kwenye michuano ya kimataifa na iliondolewa mapema kwenye hatua ya mtoano na ilishinda mechi mbili tu kati ya nne.

Nabi aliondoka nchini akiwa tayari ameipa Yanga mataji mawili ya Ligi Kuu Bara mfululizo, taji moja la Ngao ya Jamii na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Pia aliiongoza kucheza michezo 49 ya Ligi Kuu Bara bila kufungwa na kati ya hiyo ilishinda 36 na kutoka sare 12 huku akiachana na kikosi hicho msimu uliopita na nafasi yake kuchukuliwa na Muagentina, Miguel Gamondi Juni 24, mwaka jana.

Wydad ipo nafasi ya tano kwenye msimamo baada ya kukusanya pointi 37 kwenye mechi 24 ilizocheza ikishinda 10, sare saba na kupoteza mara saba.

SOMA NA HII  AUCHO AIGOMEA YANGA...WAARABU WAMSHAWISHI KWA MKATABA MNONO...