Home Habari za michezo HUYU NDIO BENCHIKHA SASA….ALICHOKIFANYA CHAWASHANGAZA MAKOCHA SIMBA…

HUYU NDIO BENCHIKHA SASA….ALICHOKIFANYA CHAWASHANGAZA MAKOCHA SIMBA…

Habari za Simba leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchika ameweka kikao cha dharura na benchi lake la ufundi kilichodumu kwa dakika 12, baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara wa Simba dhidi ya Mashujaa FC kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam, Wekundu wa Msimbazi ikishinda mabao 2-0

Benchikha aliwazuia makocha wote wanne kwa maana ya msaidizi, Farid Zemiti na kocha wa viungo Kamal Boujdjenane na baadae aliongezeka kocha wa makipa Dani Cadena, huku kocha msaidizi namba mbili, Seleman Matola akifanya mahojiano na wanahabari.

Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye mabenchi ya uwanja huo, Benchikha ndiye alikuwa mzungumzaji mkuu huku wengine wakichangia.

Baada ya mechi ya jana, Simba itaingia chimbo kujiandaa na mechi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri, mtanange utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Machi 29 mwaka huu.

SOMA NA HII  HESABU ZA SIMBA KIMATAIFA MSIMU HUU ZIMEKAA NAMNA HII....