Home Azam FC RASMI….AZAM FC ‘WAMSUSA’ DUBE….WAMFUNGIA MILANGO ASIRUDI TENA CHAMAZI…

RASMI….AZAM FC ‘WAMSUSA’ DUBE….WAMFUNGIA MILANGO ASIRUDI TENA CHAMAZI…

Habari za Michezo

Uongozi wa Azam FC umesemna kuwa hakuna tena nafasi kwa Mshambuliaji wa timu hiyo, Prince Dube kurejea katika kikosi na kuanzia sasa umefunga mjadala wake hadi atakapokamilisha uvunjaji wa mkataba.

Kauli hiyo ya Azam FC imekuja muda mfupi baada ya kuripotiwa kuwa Dube ana mpango wa kurejea kikosini ili kuungana na wenzake baada ya mwanzoni mwa juma hili kukutana na kocha Yousouf Dabo na kufanya naye mazungumzo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Azam FC zimelithibitisha kuwa vigogo wa timu hiyo wamepiga marufuku kwa Dube kuhudhuria mazoezi au kushiriki shughuli zozote za timu hiyo na wanachohitaji ni mchezaji huyo kulipa kiwango wanachohitaji kwa ajili ya kuvunja mkataba wake.

“Hili jambo limewaudhi sana viongozi wa juu wa Azam FC ambao wametoa agizo kuwa Dube asiruhusiwe kuwepo kwenye timu hadi pale atakapokamilisha suala la kuvunja mkataba wake, iwe kwa yeye mwenyewe kuleta fedha ambazo zinatakiwa au klabu inayomtaka ije mezani.

“Wanafahamu ujanja ambao umeanza kutumika hivyo hawataki kuruhusu utokee kwani utaivuruga timu na isitoshe hata wachezaji wenzake hawajafurahishwa na hicho anachokifanya kimesema chanzo kutoka Azam FC.

Hilo limethibitishwa na Afisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ kwa kusema kuwa wamefunga rasmi ukurasa wa mshambuliaji huyo.

“Azam FC imeshafunga mjadala wa Prince Dube. Kuanzia hatutolijadili tena suala lake hadi pale kile ambacho Azam FC inachokihitaji kitatimizwa.

“Dube bado hajarejea na hatorejea kikosini na ukurasa wake na Azam FC umeshafungwa rasmi,” amesema Zaka.

Juzi Dube alizungumza kwa kifupi kuwa mengi atayasema baada ya sakata lake na klabu hiyo kumalizika.

Kuna mambo mengi hamuyajui, wakati ukifika mtayajua kwa sasa niacheni kwanza nitafakari,” amesema Dube.

SOMA NA HII  RASMI..MOSES PHIRI AVUNJA UKIMYA KUHUSU KUDAIWA KUJIUNGA NA YANGA...AWATAJA CHAMA ,BWALYA NA FEI TOTO...