Home Habari za michezo TYR AGAIN:- KAMA AL AHLY WALIPATA BAHATI DAR….NA SISI TUNAWEZA KUPATA BAHATI...

TYR AGAIN:- KAMA AL AHLY WALIPATA BAHATI DAR….NA SISI TUNAWEZA KUPATA BAHATI MISRI…

Habari za Simba

Baada ya juzi usiku Simba kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka Al Ahly mchezo wa mkondo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Mwenyekiti wa bodi ya klabu hiyo Salim Muhene amevunja ukimya na kusema kuwa safari bado iko ‘live’.

Try Again amesema kuwa bado Simba hawajakata tamaa katika kuhakikisha wanasonga mbele hatua ya nusu Fainali huku wakiahidi kufanya maajabu katika mcheo wa mkondo wa Pili nchini Misri.

“Bahati haiwezi kuwa kwao kila siku, leo imekuwa bahati kwao, kesho inaweza kuwa kwetu, cha msingi kuwa na morali, umoja, upendo na kujiandaa, hatuwezi kwenda kushinda ugenini kama tutakata tamaa. — Mwenyekiti wa Bodi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’

“Mimi naamini kwa timu tuliyonayo, kwa nyinyi mlivyo mimi naamini kabisa tunaenda kupata ushindi, tusikate tamaa hata kidogo morali yetu iwe juu kabisa kupita hii tuliyokuwa nayo mimi naamini mnaweza kufanya hivyo na tukapata ushindi ugenini.”

SOMA NA HII  KISA SARE MBILI MFULULIZO AKIWA KWENYE BENCHI....KAZE AJISHTUKIA YANGA...ATAKA MABADILIKO...