habari za simba-Ateba
Habari za Simba Leo

LEONEL ATEBA APANDISHA MZUKA…ANATAKA MAKOMBE SIMBA

Abubakar September 28, 2024 5:28 pm

STRAIKA mchana nyavu Leonel Ateba ameweka wazi kwamba msimu huu pale Msimbazi kuna kombe linatua na haitashangaza kwamba watalichukua kutoa wapi, ingawa kwa sasa yaliyo wazi ni yale yasiyo na mwenyewe hadi sasa ni lile la Ligi Kuu Bara na la Shirikisho (FA).

Ateba amejiwekea malengo binafsi ya kuhakikisha anajitoa kuona Simba inapata mafanikio katika michuano ya ndani na ile ya kimataifa.

Kwa misimu mitatu iliyopita, Simba imeshindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho, huku katika michuano ya kimataifa imekuwa ikiishia hatua ya robo fainali kwa misimu mitano kati ya sita iliyocheza na safari hii ikiwa ni msimu wa saba imeshatinga makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Ateba alisema kuwa; “Nataka kuwa sehemu ya mafanikio ya Simba, hivyo nipo tayari kutoa zaidi ya asilimia 100 kwa ajili ya timu, nikiwa kama mshambuliaji kwa kuwajibika kufunga.”

Aliongeza katika kufanikisha hilo amekuwa akifanya mazoezi kwa nguvu huku nikijaribu kuwasoma wachezaji wenzake ili iwe rahisi katika uchezaji wake uwanjani na kutimiza malengo hayo kwa manufaa klabu hiyo.

KAZI IMEANZA… GAMONDI AWAITA CHEMBA DUBE NA MZIZE CAF KUFUTA KOMBE LA SHIRIKISHO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “LEONEL ATEBA APANDISHA MZUKA…ANATAKA MAKOMBE SIMBA”

  1. […] Jiji itaialika Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ikiwa ni muendelezo wa Ligi Kuu, huku ikiwa na rekodi mbaya […]