Home Habari za michezo YANGA WAIIGA MFUMO WA SIMBA KWENYE KUONGOZA KLABU…ENG HERSI AFUNGUKA A-Z….

YANGA WAIIGA MFUMO WA SIMBA KWENYE KUONGOZA KLABU…ENG HERSI AFUNGUKA A-Z….

Habari za Yanga leo

KLABU ya Yanga imeteua kamati ya watu wanne, inayoongozwa na Mwenyekiti Alex Mgongola kuendelea kusimamia sehemu ilisalia ya mchakato wa mabadiliko ya klabu hiyo.

Wajumbe walioteulizwa watakaokuwa chini ya Mgongolwa, ni Raymond Wawa , Ivan Torino na Eliakim Maswi ambao watasimamia katika mchakato huo ambao umebakia sehemu chache kukamilika.

Rais wa klabu hiyo, Hersi amesema maendeleo ya mfumo wa mabadiliko ya klabu ya Yanga, ambao ni kiungo kikubwa cha kwenda katika mafanikio.

Amesema kwa kipindi chote walifanikiwa katika mchakato huo na kupiga hatua kubwa na wanaimani kamati hiyo itamalizia sehemu iliyosalia na wanatarajia watakaoingia katika bodi kila mmoja atakuwa na haki.

“Hatua tunayoendea sasa ni kufungua Kampuni, kufanya tathimini ya mali za klabu ambayo tutaangalia itatoa vitu gani kuja kwenye kampuni na kuhusu kuuza utaratibu wa hisa,” amesema Hersi.

Ameongeza kuwa baada ya mchakato wanatoka wajumbe watano katika klabu kwa ajili ya kuuza asilimi 49 na hatua ya mwisho ambayo imefanyika ni kuhamisha majukumu yao kwenda katika bodi.

“Kwenye hiyo hisa 49, hakuna mtu mmoja kumiliki na lazima wawe watu wanne na kila mmoja atapata 12.25, kwenye bodi itakuwa na watu tisa ambapo watano wanatoka klabuni na wawekezaji wanatoa wanne,” amesema Rais huyo.

Ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa mchakato huo wanatarajia mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo kwa siku za usoni kutokana na kuendeshwa kisasa.

Hersi amesema ndio klabu kogwe ndani ya Taifa hili na kwa heshima hiyo, inepita safari ndefu kwa kupita milima na mabado hadi kufikia mafanikio yaliyopo sasa.

Amesema kuwepo kwa wanachama wengi au mashabiki basi kuwepo na thamani ya uwepo watu hao, Kipindi cha nyuma kulikuwa na Yusuph Manji alipambana kufikisha yanga katika mafanikio lakini baada ya kupata Changamoto mambo yote yakasimama.

“Hilo lilikuwa funzo na kuna watu wakafikiria kuweza kuondoa katika mfumo wa klabu ya kuendesha kizamani na kwenda kisasa kipindi hicho alikuwepo Mwenyekiti Mshindo Msola.

Aliunda kamati na ilifanya kazi kubwa ya kutafuta elimu na taalum ili kupata mafunzo ya kuweza kutuondoa hapa tulipo na kwenda kupata mfumo wa kisasa wa uendeshaji wa mpira,” amesema.

Hersi amesema kuna mambo matatu ambayo wameyafanyia kazi ikiwemo eneo la imiliki la klabu nyuma ilikuwa inamilikiwa na wanachama kwa asilimia 100, mfumo mchanganyika ambapo asilimia flani kumilikiwa na wanachama na taasisi fulani.

“Tulipendekeza asilimia 51 za wanachama na 49 wawekezaji, Mfumo wa uongozi wa klabu, kamati ilipendekeza kuwa klabu ilikuwa inaongoza na nguzo moja, Baada ya kujifunza na kuja na mifumo ya nguzo tatu ili moja ibaki kama ilivyo kuwepo kwa kamati ya utendaji.

Ya pili mfumo wa kutengeneza kampuni mpya itakayojengwa na klabu ambayo itamiliki asilimia 100 ambayo itauza asilimia 49 kwa wawekezaji, Kampuni itaundwa na watu 9 na kutoa wawakilishi watano kutoka kwa klabu na watakaonunua watatoa wanne,” amesema Hesri.

Ameongeza kuwa kati ya hapo Mwenyekiti anatoka katika klabu ambaye atakuwa na Rais na mtu wa pili atatoka katika baraza la wadhamini na watatu atakuwa katibu mkuu ambaye ataajiriwa na wala sio Mtendaji Mkuu.

“ Baada ya yote hayo chini ya Bodi hiyo itakuwa na Mtendaji Mkuu hivyo yule CEO wa klabu atatoka katika klabu na kwenda katika bodi ya kampuni ambayo itaendesha shuhuri zote za klabu,” amesema Hersi.

SOMA NA HII  KUHUSU KUONGEZA MKATABA YANGA...AZIZ KI KAANIKA HAYA MAPYA LEO...