Home Habari za michezo KUHUSU CHE MALONE KUTAKA KUSEPA SIMBA …WAKALA WAKE KAANIKA A-Z MCHONGO ULIVYO…

KUHUSU CHE MALONE KUTAKA KUSEPA SIMBA …WAKALA WAKE KAANIKA A-Z MCHONGO ULIVYO…

Habari za Simba leo

Wakala wa Beki wa Klabu ya Simba, Che Malone, Amadou Fontem Tigana, amesema beki huyo hajasema kuwa haipendi Simba na wala hajasema kuwa anataka kuondoka Simba, bali watu wamemtafsiri vibaya mchezaji huyo.

Tigana ameyasema hayo wakati akizungumza na ITV kwa njia ya simu, ambapo amesisitiza kuwa taarifa hizo ni uzushi kwani ametafsiriwa vibaya baada ya kusema kuwa atacheza Kwa juhudi ili klabu kubwa kama Simba zimnunue.

Ufafanunuzi huo wa Tigana unafuata, baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa mchezaji huyo amefanya mahojiano kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu ujao na kwamba tayari ameandika barua ya kuondoka Simba na kwamba anatala akatafute changamoto kwenye timu kubwa.

Malone aliyetua kikosini msimu huu akisaini mkataba wa miaka miwili amewaambia marafiki zake wa karibu ikiwemo wakala wake, amtafutie timu nyingine kwani anataka kufanya makubwa zaidi kabla ya kustaafu.
Hata hivyo, beki huyo aliyetua Simba SC akitokea Cotonsport ya Cameroon amethibitisha hilo katika mahojiano na kituo cha Canal- Sports cha Ufaransa kupitia kipindi maalumu kinachohusu soka na wachezaji wa Afrika, akisema anafikiria kuondoka Simba SC mwisho wa msimu.

“Nilicheza Cotonsport kwa misimu miwili na kutwaa taji la Ligi mara mbili mfululizo, nikataka kupata changamoto mpya. Nacheza soka ili kupata maendeleo na sio kubaki katika eneo moja tu.” amesema Malone na kuongeza.

“Ndoto yangu ni kucheza kwenye klabu kubwa na naamini msimu ujao nitakuwa timu kubwa, kwenye soka miujiza pekee ni nidhamu na kufanya kazi kwa bidii. Simba SC ni hatua nyingine kwangu kwa kuwa ndoto yangu ni kucheza kwenye moja ya klabu kubwa duniani.” amesema Che Malone

Meneja Habari na Mawasilino wa Simba SC, Ahmed Ally alipoulizwa juu ya taarifa hizo amesema kwa sasa timu inajali zaidi michezo inayofuata ya Ligi Kuu hivyo jambo la kusajili au kuondoka kwa wachezaji wapya limeachwa kwa kocha ndiye atafanya maamuzi.

Usajili wote tumemuachia kocha, yenye ndiye ataamua nani aondoke au kubaki kikosini kutokana na aina ya timu anayoitaka kwa msimu ujao hivyo hayo tuayaache kwanza tuzingatie zaidi mechi zijazo, alijibu Ahmed alipoulizwa kuhusu suala hilo.

Kama Malone na Inonga wataondoka Simba SC kwa pamoja, basi timu hiyo itatengeneza pesa ndefu kutokana na thamani ya kuwang’oa kikosini hapo kutokuwa chini ya 600 milioni kwa kila mmoja lakini itapata kibarua cha kuingia sokoni kushusha majembe mapya yatakayoziba nafasi zao.

SOMA NA HII  GAMONDI SIO KINYONGE AJA NA HILI KIGALI