Home Habari za michezo NI KWELI BABACAR SARR KATATUA SHIDA YA KIUNGO SIMBA?….UKWELI WA KUJUA HUU...

NI KWELI BABACAR SARR KATATUA SHIDA YA KIUNGO SIMBA?….UKWELI WA KUJUA HUU HAPA…

Habari za Simba leo

Simba ilipoamua kumsajili Babacar Sarr katika dirisha dogo la usajili la Januari ilikuwa imebaini tatizo ambalo lipo kwenye kikosi chake msimu huu.

Tatizo hilo ni safu yake ya ulinzi kutopata ulinzi wa kutosha kutoka kwa kiungo wa ulinzi au namba sita kwa vile wachezaji watatu ambao walikuwa wakitumika kwa nyakati tofauti katika nafasi hiyo kiasili walikuwa hawaimudu.

Viungo hao watatu ambao ni Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin wameonekana sio aina ya wachezaji wanaoweza kuipa ulinzi mkubwa safu ya ulinzi kwa sababu wote huwa hawawezi kutulia sehemu moja.

Hawa watatu ni viungo ambao wanapenda kutembea na mpira kutoka katika eneo la ulinzi kwenda kusaidia upande wa mashambulizi na kuna nyakati utawaona wakiwa juu zaidi na sio mbele ya ukuta wa timu.

Sasa lengo la kusajiliwa kwa Babacar Sarr lilikuwa ni jema kwamba yeye acheze mbele ya ukuta kuhakikisha upo salama na asisogee juu mara kwa mara ili kutoa uhuru ama kwa Ngoma, Mzamiru na Kanoute atakayepangwa nae awe anafanya hivyo.

Lakini imekuwa tofauti kwani Sarr ameonekana kutotimiza majukumu ya msingi ya nafasi yake na kuiweka matatani safu ya ulinzi ya Simba mara kwa mara na kuifanya iwe inaruhusu mabao mepesi sana.

Amekuwa mzito kurudi katika eneo lake pindi anaposogea mbele kusaidia mashambulizi lakini amekuwa hatimizi wajibu wa kudhibiti kiungo au mshambuliaji ambaye anaonekana kuwa hatari kwa timu yake ambaye anakuwepo katika nafasi ambayo yeye Sarr ndio anapaswa kumkaba kama kiungo mzuiaji.

Ukitazama bao la kwanza ambalo Simba ilifungwa na Al Ahly katika mechi ya ugenini ya hatua ya robo fainali wiki iliyopita unaweza kupata picha halisi ya jinsi Sarr anavyoirudisha Simba kwenye tatizo lilelile la kutokuwa na namba sita wa kueleweka.

Anthony Modeste anapokea mpira akiwa amedhibitiwa na beki mmoja wa Simba, anampasia Amr El Soleya ambaye alikuwa huru katika eneo ambalo alipaswa kudhibitiwa na Sarr na nyota huyo wa Al Ahly anaukwamisha mpira wavuni pasipo bughudha yoyote.

SOMA NA HII  GEITA GOLD:TUNAWAHESHIMU YANGA ILA TUNATAKA POINTI TATU