Habari za Michezo leo
Habari za michezo

ALLY KAMWE:- MECHI YETU NA SIMBA TUMEIITA WAZEE DAY…AMEFUNGUKA HAYA

Marce Ben Komba April 16, 2024 10:09 am

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wameliita pambano lao na Simba SC jina la Wazee Day.
Yanga SC wamekuwa na utamaduni wa kutoa majina katika michezo yao ya nyumbani ili kutengeneza hamasa.

“Hii mechi kwa heshima kubwa kabisa, kwa kutambua umuhimu wa mchezo na upekee wake, tumeamua mchezo huu wa Jumamosi tuwakabishi wazee wetu.

Huu mchezo ni special dedication Wazee Day. Wazee wa Yanga wote duniani hii mechi ni ya kwenu, tukifungwa ni nyie.

“Wazee wangu wa Yanga tumeona tuwaheshimishe kwenye mchezo huu, mje kwa wingi na dua zenu zitasaidia kupata matokeo chanya kwenye huu mchezo,” amesema Kamwe.

Pambano hilo la Ligi Kuu Bara litachezwa Jumamosi, Aprili 20, 2024 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam huku Yanga wakiwa wenyeji wa mchezo huo.

VIFAA VIPYA MSIMBAZI HIVI HAPA…..NI MASHINE ZA KAZI HASWA….BENCHIKHA APIGA TIKI…. SHABIKI SIMBA:- HATUWEZI KUIFUNGA YANGA…TUNAKWENDA KUDHALILIKA…TUTAKULA KIPIGO KIZITO