Habari za Yanga leo
Habari za Yanga

KUMBE STAA HUYU YANGA..ALIKUWA ANALIPWA LAKI SITA TU…APANDISHIWA HADI 12M

Marce Ben Komba April 16, 2024 10:59 am

Kwa kipindi cha hivi karibuni Ligi yetu imekuwa na ubora mkubwa hasa baada ya klabu mbili za Simba na Yanga kuanza kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.

Jambo hili limewavutia nyota wengi kuja kuitumikia Ligi hii licha ya ubora wa Ligi kuongezeka bado pia maslahi kwa nyota wengi yameongezeka.

Wakala Ronnie Santos ambaye alisimamia dili la Mlinzi wa klabu ya Yanga Gift Freddy amesema kuwa wakati anamtafuta mchezaji huyo huko alipokuwa alikuwa akilipwa laki sita pekee lakini kwa sasa akiwa na Yanga analipwa zaidi ya million 12.

“Gift Fred akiwa anaitumikia SC Villa alikuwa analipwa 600k kwa Mwezi, nikamfanyia mpango wa kulipwa zaidi ya 12M kila Mwezi ndani ya Young Africans na jambo hilo likafanikiwa.”

BOSI YANGA AWAGEUKIA MASHABIKI…”HUWEZI KUSEMA TUMESHINDA…VIONGOZI WA MATAWI KIKAANGONI AHMED ALLY:- HATA TUKICHEZA NA TIMU NDOGO LAZIMA TUFUNGWE…MAKOSA YANAJIRUDIA..AMEFUNGUKA HAYA