Azam FC
Azam FC

AZAM FC YAVUTA KITASA HICHI KIPYA…KWA BEKI HUYU MJIPANGE…ATAMBA MASHINDANO YA CHAN

Marce Ben Komba April 19, 2024 11:25 pm

Azam FC imefikia makubaliano ya kumnunua beki wa kimataifa wa Mali, Yoro Mamadou Diaby, kutoka Kituo cha Soka cha Yeleen Olympique cha nchini humo.

Mlinzi huyo wa kati ambaye alikuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Stade Malien de Bamako iliyofika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, atajiunga rasmi na Azam FC kuanzia msimu ujao wa 2024/25.

Yoro amezichezea timu zote za vijana za taifa za Mali, kuanzia ile ya chini ya 17, chini ya miaka 20 na chini ya miaka 23 na alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshiriki CHAN, mwaka 2022 nchini Algeria.

WAKILI YANGA:- “SIMBA INA WACHEZAJI WALIOZOEA KUMKABA RONALDO…AMEFUNGUKA HAYA UHURU SELEMAN:- MNAMPAMBA LOMALISA NI BEKI WA KAWAIDA SANA…MADOGO ACHENI USELA