MSECHU:- SIMBA WAKIIFUNGA YANGA MNITTE PENDO...AWAPA TAHADHARI HII MASHABIKI WA MSIMBAZI
Michezo

MSECHU:- SIMBA WAKIIFUNGA YANGA MNITTE PENDO…AWAPA TAHADHARI HII MASHABIKI WA MSIMBAZI

Marce Ben Komba April 19, 2024 10:37 pm

Msanii wa Bongo Fleva na msanii maarufu wa Bongo Fleva, Peter Msechu amesema kuwa iwapo kikosi cha Yanga kitafungwa kesho dhidi ya watani wao Simba SC basi abadilishiwe jina badala ya kuitwa Peter aitwe Pendo.

Kesho Yanga wanatarajia kushuka dimbani kuvaana na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC huku wakipewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo kutokana na uwezo wao.

“Kwa kifupi ukitaka kupunguza stress na kuwa na maisha marefu duniani, shabiki wa Simba kesho kaa nyumbani kwa sababu unaweza kupaona nyumbani kwako kutoka uwanjani ni kama unaenda mkoani, huo ndio ujumbe wangu.

Kwenda patakuwa karibu lakini kurudi patakuwa ni mbali sana.
“Yani Yanga akifungwa kesho na Simba, mimi si naitwa Peter? Basi niitwe Pendo, basi,” amesema Peter Msechu.

YANGA ;- SIMBA NI KLABU TAJIRI ZAIDI….WANAMCHEZAJI ALIYEMKABA RONALDO…. WAKILI YANGA:- “SIMBA INA WACHEZAJI WALIOZOEA KUMKABA RONALDO…AMEFUNGUKA HAYA