FIGISU ZATAWALA SOKA LA AFRIKA...TIMU YAFANYA MAZOEZI AIRPORT...YAZUILIWA KUTOKA UWANHANI
Habari za michezo

FIGISU ZATAWALA SOKA LA AFRIKA…TIMU YAFANYA MAZOEZI AIRPORT…YAZUILIWA KUTOKA UWANHANI

Marce Ben Komba April 21, 2024 10:24 am

Kikosi cha timu ya RS Berkane kimelazimika kufanya mazoezi yao katika Uwanja wa Ndege nchini Algeria baada ya kuzuiliwa kutoka katika uwanja huo. Pichani ni Berknane wakifanya mazoezi ya viungo.

Chanzo cha kuzuiliwa inaelezwa kuwa kutokana na jezi walizovaa zina nembo ya Ramani ya nchi yao ya Morocco ambapo waliambiwa na maofisa nchini Algeria kuwa wafunike Bedera ya nchi hiyo kwa stika lakini wakagoma.

Kumbuka Berkane watakuwa na kibarua cha nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kesho Jumapili dhidi ya Mabingwa watetezi wa michuano hiyo USM Alger.

Berkane wamekuwa wakizitumia jezi hizo tangu wameanza hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na hawakuwahi kubughudhiwa na nchi yoyote.

FT: YANGA 2-1 SIMBA SC…..GUEDE, FREDY WAINGIA KWENYE REKODI YA DERBY….UBINGWA BADO 6 TU… KAKOLANYA AGOMEA WITO WA KAMATI YA NIDHAMU SINGIDA BS…HAMNITTENDEI HAKI ISHU NZIMA HII HAPA