Habari za Simba leo
Habari za michezo

KARIAKOO DABI YAWAPA SAPRAIZI HII GAMONDI NA BENCHIKHA…WABAKI MIDOMO WAZI

Marce Ben Komba April 21, 2024 11:28 am

Unaweza kusema ni kama makocha wa timu zote mbili, Miguel Gamondi wa Yanga na Abdelhak Benchikha wa Simba wamekutana na sapraizi, baada ya kulazimika kufanya mabadiliko ya mapema zaidi.

Kwa kawaida, mabadiliko ya wachezaji kwenye mechi hufanyika kiufundi, lakini jana makocha hao walilazimika kuyafanya mapema bila ya kutarajiwa.

Alianza Gamondi kufanya mabadiliko ya kumtoa Joyce Lomalisa dakika ya 6 ya mchezo huo, baada ya beki huyo wa kushoto kuonekana kuugulia nyama za paja, nafasi yake ikachukuliwa na Nickson Kibabage.

Dakika 5 baadaye kwa maana ya ilipofika 11 tangu kuanza kwa mchezo huo, Benchikha naye alilazimika kumtoa Henock Inonga na kuingia Hussein Kazi.

Inonga alionekana mapema tu akichechemea tangu kuanza kwa mchezo huo ikionekana akisumbuliwa na misuli, lakini baadaye alipokuja kugongana na Clement Mzize, ikawa ndiyo mwisho wa kuendelea. Akatolewa.

KUMBE PACOME ALIMLILIA GAMONDI KABLA YA DABI…BOSS YANGA AFUNGUKA ISHU NZIMA A-Z PAMOJA NA KUWATUNGUA SIMBA JANA….GAMONDI KAIBUKA NA HILI KWA YANGA….