IMEELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha huenda msimu ujao akaea sehemu ya benchi la ufundi na kuendelea kukinoa kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi baada ya kupata ofa ya kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Algeria.
Taarifa za uhakika kuwa baada ya kupokea Ofa hiyo, Benchikha ameutaka uongozi kutoendelea kukinoa kikosi cha Simba kwa msimu ujao na kwenda kutafuta changamoto zingine ikiwemo dili hilo ambalo lipo mezani.
Mtoa habari huyo alisema uongozi umeridhia maombi yake licha ya Mwekezaji, Mohammed Dewji kutaka kuendelea na kocha Benchikha kwa msimu mwingine.
“Suala la Benchikha kubaki kwa msimu uliopita imekuwa ngumu licha ya maombi ya mwekezaji huyo kugonga mwamba na tayari mchakato wa kupata kocha mpya umeanza mapema.
Msimu wa 2024/25 anakuja kocha mwingine, Benchikha anakwenda kufundisha timu ya taifa ya Algeria na pree season kutakuwa na kocha mpya mambo yatakuwa. yamekamilika yote, bonge la kocha sijui anatoka nchi gani,” alisema mtoa habari huyo.
Aliongeza kuwa mchakato kumpa mrithi wa Benchikha umeanza mapema na anapoondoka kocha huyo wawe tayari kumtambulisha na kuanza na timu mapema ikiwemo kwenda na timu Pre Season na kushiriki katika usajili wa nyota wapya
Mtoa habari huyo alisema mchezaji yoyote wakitaka kumsajili lazima wajumbe ambao wako kwenye kamati ya kumshauri Mo Dewji (hawakupenda kuyaandika majina yao gazeti) waende nae kwa Mwekezaji huyo kwa ajili ya kusaini mkataba.
Alieleza kuwa wameanza kufanya kazi kimya ikiwemo suala la kocha mpya pamoja na wapo kwenye program mpya kwa ajili ya kusaka wachezaji kwa ajili ya usajili kwa msimu ujao.