NI BAADA YA KUCHUKUA KOMBE...ZIMBWE JR ATAMBA LIVE.....KUMBE AWEKA REKODI HII
Habari za michezo

NI BAADA YA KUCHUKUA KOMBE…ZIMBWE JR ATAMBA LIVE…..KUMBE AWEKA REKODI HII

Marce Ben Komba April 28, 2024 12:04 pm

Beki wa pembeni wa Simba SC, Mohamed Hussein amesema anajivunia kubeba makombe yote ya nchi hii kwa nyakati tofauti.

Mohamed ameyasema hayo jana mara baada ya kuibuka washindi katika mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano.

“Furaha yangu ni kuchukua kombe la muungano ambalo nilikuwa nalisikia tu kwenye historia ya mpira wetu kipindi nipo mdogo, namimi nimeingia kwenye hiyo historia, kwa ufupi nimechukua makombe yote ya nchii hii, Shukrani Fans wetu endeleeni kutusapoti,” aliandika Mohamed Hussein aka Zimbwe Junior.

USHINDI KWA KILA HATUA UKO NDANI YA EXPANSE STUDIO YA MERIDIANBET CASINO… LOMALISA KIBARUA KIPO HATARINI YANGA…KUMBE SABABU YA KUTEMWA NI HII