Home Habari za michezo DIARRA HUYOO…..TIMU KUTOKA URUSI KUTUMA OFA NONO YA KUMNG’OA YANGA MAZIMA…

DIARRA HUYOO…..TIMU KUTOKA URUSI KUTUMA OFA NONO YA KUMNG’OA YANGA MAZIMA…

Habari za Yanga leo

Vilabu Mbalimbali Vya Barani Ulaya vikiwemo Kasimpasa , Zenit Saint Petersburg na Dnipro FC vimeonesha nia ya kuhitaji huduma ya Mlinda mlango Wa Klabu ya Yanga SC, Djigui Diarra katika Dirisha kubwa la Usajili la Msimu Ujao.

Taarifa zinathibitisha kwamba vilabu viwili kati ya vitatu vilivyoonesha nia vimeshawasiliana na Management inayomsimamia Diarra na jibu walilopewa ni kusubiri mpaka mwisho wa msimu.

Diarra ambaye Mkataba wake na Yanga unaisha mwezi Mei ni miongoni mwa magolikipa wachache waliowavutia wengi kwenye michuano ya AFCON 2023 kutokana na uwezo wake wa kudaka pamoja na kuanzisha mashambulizi kutoka nyuma.

Kagoma anukia jangwani.

Klabu ya Yanga imeanza harakati za kunasa saini ya kiungo mkabaji wa Klabu ya Singida Fountain Gate, Yusuph Kagoma kwa ajili ya kuimarisha safu yao ya kiungo msimu ujao.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa, Kocha Miguel Gamondi amekuwa akimfuatilia Kagoma katika mechi nyingi na amevutiwa na uwezo wa kiungo huyo na anataka ajumuishwe kwenye kikosi chake msimu ujao.

Tayari Injinia Hersi ameshaanza mazungumzo na mchezaji huyo kuona uwezekano wa kumchukua kama mbadala wa Zawadi mauya ambaye mkataba wake unamalizika na hayupo kwenye mipango ya timu hiyo msimu ujao.

Yanga imepanga kumsajili Kagoma kwa usajili wa ndani huku jicho lao kubwa likiwa kwa mshambuliaji aliyeachana na Azam FC hivi karibuni, Prince Dube raia wa Zimbabwe.

SOMA NA HII  WAKATI WAKIENDELEA KUSHINDA KILAINI MECHI ZAO....MAYELE 'AAMUA KUJILIPUA' YANGA....