Home Habari za michezo PAMOJA NA KUKOSA PENATI JUZI…AZIZI KI KAVUNJA UKIMYA KINACHOENDELEA YANGA…

PAMOJA NA KUKOSA PENATI JUZI…AZIZI KI KAVUNJA UKIMYA KINACHOENDELEA YANGA…

Habari za Yanga leo

Kikosi cha Yanga kipo njiani kurejea nchini baada ya usiku wa jana kutolewa katika hatua ya rono fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mikwaju ya penalti 3-2 na Mamelodi Sundowns katika mechi kali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Luftus Versfeld jijini Pretoria, Afrika Kusini huku kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Stephane Aziz KI akivunja ukimya juu ya mchezo huo aliokosa penalti ya kwanza.

Aziz Ki aliyeupiga mwingi katika mchezo huio ambapo pia mpira wa shuti kali alililopiga kutokana na pasi ya Kennedy Musonda kuonekana kuangukia ndani ya lango la Mamelodi katika kipindi cha kwanza, lakini likakataliwa na V.A.R amesema licha ya kupoteza mchezo huo, lakini Yanga imeonyesha kuwa ni timu bora Afrika.

“Benchi la ufundi na sisi wachezaji tumeonyesha kuwa sisi ni timu kubwa, timu ambayo ina dhamira ya kurudisha klabu hizi katika viwango vya juu kabisa vya Afrika,” alisema Aziz KI na kuongeza;

“Kwabahati mbaya haikuwa hivyo, lakini hatutampa mtu nafasi kama timu na mashabiki kwa mara nyingine tena mlituunga mkono kutoka kila sehemu mlisafiri kutoka sehemu zote za Tanzania ili muwepo kwenye mechi hii na nadhani mmeondoka kwa kiburi kwamba wachezaji wenu tulipambana kuhakikisha tunawapa matokeo mazuri.”

Aziz Ki alisema kucheza na Mamelodi sio kitu rahisi, lakini wao walipambana katika mechi zote mbili nyumbani na ugenini wakionyesha nia yao ya kufika mbali bila kujali vikwazo.

“Msimu huu hatujafanikiwa licha ya mapambano yote tunawaahidi tutarudi imara zaidi msimu ujao tutarudi tukiwa na nguvu zaidi na tutajifunza kutokana na kushindwa kwetu leo,” anasema kiungo raia wa Burkina Faso na kuongeza;

“Nina maumivu makali ya kushindwa kuisaidia timu kufika mbali zaidi ila namshukuru Mungu siku zote katika nyakati nzuri na mbaya maana yeye pekee ndiye mkuu wa kila kitu na nyie wenzangu mnajua kuwa mimi najivunia nyinyi na kama nilivyosema hatutawahi kuinamisha vichwa vyetu hata tukikutana na timu gani, tumepoteza ndio, lakini tunatoka na vichwa juu kwa sababu sisi ni timu nzuri na tunakwenda kufanya kazi ili kufikia malengo yetu msimu ujao.”

Pia alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango mkubwa alioutoa kwao kipindi chote cha mashindano huku akimuahidi kuwa walikwensa Afrika Kusini kama mashujaa na wanarudi Tanzania kama shujaa wakiwa na mafunzo mengi ya kuhakikisha wanakuwa bora zaidi msimu ujao.

Katika mchezo wa mchezo huo wa jana usiku, Yanga ilipoteza penalti tatu ikiwamo ya kwanza iliyopigwa na Aziz KI, kisha Dickson Job na Ibrahim Bacca huku, Augustine Okrah na Joseph Guede wakitupia zao, lakini haikuisaidia Yanga kupoteza kwani wenyeji walitupia zao tatu na kupoteza moja.

Kwa matokeo hayo, Mamelodi inaungana na Al Ahly ya Misri ambao ni watetezi wa taji la michuano hioyo kufuzu nusu fainali sasa zinasubiri matokeo ya mechi za leo usiku za marudiano za robo fainali kati ya Petro Atletico ya Angola na TP Mazembe ya DR Congo na ile ya Asec Mimosas ya Ivory Coast dhidi ya Esperance ya Tunisia. Katika mechi za kwanza timu hizo zote zilitoka suluhu na mshindi wa mechi ya Petro na Mazembe ndio itakayocheza na Al Ahly na ile Mamelodi itasikilizia kujua itavaana na Asec Mimosas au Esperance.

SOMA NA HII  YUSUPH ATHUMAN WA YANGA ANAHITAJI KUFUNGA MABAO YAKUTOSHA