Home Habari za michezo HIZI HAPA SABABU ZA SKUDU KUFUNGIWA MILANGO YA KUCHEZA YANGA YA GAMONDI…

HIZI HAPA SABABU ZA SKUDU KUFUNGIWA MILANGO YA KUCHEZA YANGA YA GAMONDI…

Habari za Yanga SC

Skudu Makudubela anapata wakati mgumu kupenya kwenye Kikosi cha kwanza cha Miguel Angel Gamondi kwa sababu kocha huyu ni muumini wa mchezaji ambaye ana faida wakati timu yake haina mpira mguuni.

Gamondi anataka mchezaji ushiriki kusaka mpira pindi tuu ukipotea kwenye himaya yenu, jambo kubwa unalotakiwa kufanya ni kuanza kumnyima mpinzani wako nafasi ya kupitisha mpira ukiwa kwenye himaya yake .

Skudu hawezi kufanya kazi hiyo kwa sababu yeye ana enjoy zaidi kucheza Soka Mpira ukiwa katika himaya yake na ukimpotea Hana uwezo wa kuutafuta.

Nyota huyu amekosa nafasi ya kucheza Yanga Kwa sababu ya sababu za ki mfumo tuu lakini si kiwango chake kidogo, yule Maxi Nzengeli, Augustine Okrah na nyota wengine wote wanaocheza pembeni pale Yanga Wana faida hata timu yao ikipoteza umiliki wa mpira.

SOMA NA HII  SEHEMU YA CV YA KOCHA MPYA YANGA HII HAPA