Home Habari za michezo KUHUSU SIMBA, YANGA KUFUZU NUSU FAINAL LEO….MCHAMBUZI AWEKA UNAFKI PEMBENI…

KUHUSU SIMBA, YANGA KUFUZU NUSU FAINAL LEO….MCHAMBUZI AWEKA UNAFKI PEMBENI…

Habari za Michezo leo

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia Clouds FM, Master Tindwa amezitabiria Simba na Yanga kufuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa asilimia chache.

Master ametoa utabiri wake ikiwa ni siku chache tu zinesalia kabla ya Yanga kuvaana na Mamelodi Sundowns nchini Afrika Kusini, huku Simba akivaana na Al Ahly nchini Misri.

“Kwa mtazamo wangu, Simba na Yanga zina asilimia chache sana za kuvuka hatua ya Robo Fainali kwenda Nusu Fainali kwa sababu wameshindwa kufanya vizuri nyumbani.

“Watu wengi wanasema Yanga wakipata sare ya bila kufungana bado wanakuwa wapo kwenye mchezo au sare ya magoli wanafuzu, lakini naona bado ni mlima mrefu kwao.

“Natoa asilimia 10 kwa Simba kuitoa Al Ahly na kufuzu Nusu Fainali lakini Yanga naipa asilimia 20 ya kuitoa Mamelodi Sundowns na kufuzu hatua ya Nusu Fainali,” amesema Master Tindwa, Mchambuzi Clouds FM.

SOMA NA HII  KAMATI YA MASAA 72 YATOA TAARIFA KUHUSU SIMBA V YANGA