Home Habari za michezo KIBABAGE NA YANGA MAMBO NI BULL BULL…SIMBA WAPIGWA KIKUMBO CHA MWAKA…

KIBABAGE NA YANGA MAMBO NI BULL BULL…SIMBA WAPIGWA KIKUMBO CHA MWAKA…

Habari za Michezo leo

KLABU ya Yanga imefanikisha kumbakisha beki Nickson Kibabage, aliyekuwa akiichezea klabu hiyo kwa mkopo kutoka Singida Fountain Gate, baada ya kumsainisha mkataba wa miaka mitatu ya kuendelea kuitumikia.

Uongozi wa klabu hiyo umeamua kufanya hivyo baada ya mchezaji kuonyesha kiwango cha hali ya juu huku akiwa anamalizia mkataba wake wa mkopo msimu huu.

Taarifa za uhakika, ni kuwa Kibabage amesaini mkataba huo akitokea Singida Fountain Gate FC na sasa ni mali rasmi ya Yanga, ikizima ndoto za klabu ya Simba ambayo ilionekana kumhitaji kwa udi na uvumba mchezaji huyo.

Imeelezwa kuwa baada ya Simba kuhitaji huduma ya beki huyo na kupeleka ofa yao Singida Fountain Gate FC lakini Yanga wamegoma kumuachia na kupandisha dau na kufanikiwa kumpata mkataba wa miaka mitatu kusalia ndani ya kikosi cha Yanga.

“Ni kweli Kibabage amesaini mkataba w miaka mitatu na sasa anaendelea kusalia ndani ya Yanga baada ya kuwepo kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Singida Fountain Gate FC,” amesema mtoa habari huyo.

Mbali na mchezaji huyo pia Yanga wapo kwenye mazungumzo ya kumuongeza mkataba beki wao Kibwana Shomari ambaye inasemekana Azam FC wanahitaji huduma ya nyota huyo amekuwa na kiwango kizuri ndani ya kikosi cha timu hiyo.

Kwa mujibu wa Rais wa Yanga, Hersi Said kuwa wanahakikisha wanamalizana kwa kuwaongezea mikataba wachezaji wako kwenye mipango ya msimu ujao.

“Tunahitaji kuimarisha kikosi kwa ajili ya msimu ujao kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa hasa ligi ya Mabingwa kuvuka tulipoishia msimu huu, kufika huko lazima tuimarisha timu yetu kuwaongezea mikataba kwa wale waliopo tamati na baadae tuanze kutoka nje usajili mpya,” amesema Rais huyo.

Ofisa habari wa Singida Fountain Gate FC Hassan Massanza amethibitish kuwepo kwa mazungumza na uongozi wa Yanga ambao wameonyesha nia ya kumnunua mchezaji huyo.

“Ni kweli tumepokea ofa kwa klabu zote mbili lakini Yanga umeonesha interest ya kumnunua mchezaji wetu na tayari tumeshafanya nao mazungumzo, kwa sasa tupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha sehemu iliyobakia,” amesema Massanza.

SOMA NA HII  WAKATI DILI LAKE NA MAZEMBE LIKIFA NJIANI...YANGA WAFUNGUKA HATMA YA MUKOKO...WAGUSIA MKATABA WAKE..