Habari za michezo
DICKSON JOB AMVAA MUDATHIR…KUMBE SIMU YAKE IMEIBIWA…ISHU NZIMA IKO HIVI
Marce Ben Komba
May 5, 2024
8:47 pm
Mchezaji wa ‘klabu ya Yanga Dickson Job amemtania mchezaji mwenzake Mudathiri Yahya kwa kueleza kuwa simu aliyokuwa akitumia Mudathiri kupiga wakati akiwa amefunga bao imeibiwa.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Job ame-share picha akiwa na Mudathiri ikiambatana na ujumbe usemao “Simu ya Anko Mudathiri imeibiwa msione kimya ikipatikana basi itaendelea kuita
Mudathiri Yahya ni mchezaji ambaye anatumia staili ya kupiga simu baada ya kufunga bao wakati akiwa kwenye ‘mechi’.