Habari za Yanga leo
Habari za michezo

KOCHA YANGA AWALALAMIKIA BODI YA LIGI…”WACHEZAJI WANAPUMZIKA WAKIPATA MAJERAHA

Marce Ben Komba May 5, 2024 9:43 am

Kocha Mkuu wa Yanga SC Miguel Gamondi amesema licha ya ratiba ngumu ya michezo ndani ya ligi kuu kwa kucheza kila baada ya siku 3 lakini dhamira yao ni kushinda kwenye kila michezo 6 iliyosalia ndani ya Ligi Kuu Tanzania 2023-24

Gamondi amesema “tuna kalenda ngumu ya kila baada ya siku 3 na ndio maana kuna baadhi ya wachezaji nawapumzisha kwa ajili ya majeraha au kupata muda wa kupumzika lakini kuna mashabiki hawapendi au hawaelewi lakini wachezaji wanapaswa kuwa timamu kwa kila mchezo kwa asilimia 100.”

GAMONDI AWAPIGA MKWARA HUU MASHUJAA…AMEFUNGUKA HAYA A-Z MPUNGA WA UHAKIKA UKO KWENYE ODDS ZA MERIDIANBET LEO HII…TUSUA SASA..