KELVIN JOHN KUIONGOZA TAIFA STARS...MSUVA,SAMATA,ZIMBWE JR WATEMWA
Habari za michezo

KELVIN JOHN KUIONGOZA TAIFA STARS…MSUVA,SAMATA,ZIMBWE JR WATEMWA

Marce Ben Komba May 8, 2024 10:09 am

Mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Kelvin Pius John ‘Mbappe’ anatarajiwa kuongoza kikosi cha Taifa Stars kwenda nchini Saudi Arabia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan.

Ikiwa nchini humo Stars itacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Sudan kabla ya kurudi nchini kuendelea na ratiba zake nyingine.
Katika kikosi kilichoitwa na kocha Hemed Seleman ‘Morroco’ kuna namba kubwa ya wachezaji ambao ni makinda.

Kikosi kilichoitwa kina makipa Ahmed Ali Suleiman, Ally Salim na Abrahman Vuai Nassoro.

Mabeki ni Mukrim Issa Abdallah, Alphonce Mabula Msanga, Miano Danilo Van Den Bos, Gadiel Michael Kamagi, Abdulmalik Adam Zakaria, Baraka Shabaan Mtuwi, Abdulrahim Seif Bausi, Mohammed Ali Omar Sagaf.
Viungo ni Morice Michael Abraham, Khalid Habibud, Ishaka Said Mwinyi na Jabir Seif Mpanda

Washambuliaji ni Omary Abdallah Omary, Ben Anthony Starkie, Oscar Adam Paul, Tarryn Allarakhia na Ibrahim Hamad Ahmada na Kelvin.

ISHU YA UWEKEZAJI MO DEWJI NA SIMBA YAFIKA BUNGENI…”MWEKEZAJI ANALETA JANJA JANJA BOUNTY HUNTERS MCHEZO WA KASINO UNAOTOA MADINI. UPO MERIDIANBET….