Kwa mujibu wa mwandishi Micky Jr ni kuwa timu zote ambazo zimekumbana na kadhia ya kufungiwa usajili kutokana na madai mbalimbali zipo katika hatari ya kunyimwa leseni ya ushiriki wa mashindano ya kimataifa msimu ujao kama tu, hawatamalizana na wadai wao mpaka kufikia Mei 31, mwaka huu.
Kwa Tanzania miongoni mwa timu ambazo zimekutana na rungu la kufungiwa ni Mabingwa mara 30 wa ligi Kuu Bara, Yanga.
Baadhi ya wachezaji waliotajwa kuidai Yanga ni Lazarous Kambole (Zambia), Mamadou Doumbia (Mali), gael Bigirimana.
Itakumbukwa kuwa usajili wa wachezaji hao ulikuwa wa ‘kushata’ kiasi cha kufanya mitandao ya kijamii kushamiri sifa kemi kemi za wasifu wa wachezaji hao.
Hata hivyo hawakudumu na timu hiyo kulingana na kuwa na viwango vidogo kuliko ilivyotazamiwa na wengi na uongozi wa Yanga ukaamua kuwapiga chini mazima.
Yanga wamekuwa na hawana mzaha linapokuja suala la kuachana na mchezaji asiyeweza kukidhi mahitaji yao kwa wakati kwani kila msimu wanawaacha wachezaji wa namna hiyo.
Hata msimu huu inatazamiwa huenda ikaachana na wachezaji kadhaa kama , Skudu, Zawadi Mauya, Farid Musa, Nkane,