Home Habari za michezo WAKATI AYOUB ANASITASITA KUSAINI ….MAKIPA HAWA HAPA KUTUA SIMBA CHAP…

WAKATI AYOUB ANASITASITA KUSAINI ….MAKIPA HAWA HAPA KUTUA SIMBA CHAP…

Habari za Simba leo

WAKATI Simba wakiendelea kufanya mazungumzo na kipa wao Ayoub Lakred kumbakiza lakini uongozi huo umeomyesha nia ya makipa wengine wawili kwa kigeni.

Makipa hao ni uic Owono kutoka nchini Gabon na Lay {Matampi} kutoka Coastal Union ambao wameonekana kuwa sehemu mbadala wa Ayoub endapo hatoongeza mkataba kwa msimu ujao.

Kipa huyo ameonyesha uwezo mkubwa kwa msimu huu na kuitumikia klabu hiyo mwaka mmoja ambao umefikia tamati na sasa yupo huru na uongozi wa Simba kuhitaji kumuongeza mkataba mwingine.

Imeeleza kuwa viongozi wanapambana kuhakikisha wanambakiza kipa huyo kuendelea kusalia ndani ya Simba kwa msimu ujao licha ya kuanza mchakato mwingine wa kutafuata kipa mwingine wa ziada.

“Ayoub anatarajia kuondoka nchini na kwenda kwao kwa ajili ya mapumziko huku mazungumzo yakiendelea, wanapambana kuona kipa huyo anasailia tena Simba, lakini pia wanaangalia upande mwingine wa kuzungumza na baadhi ya makipa,” amesema mtoa habari huyo.

Amesema mipango yao baada ya Ayoub ni makipa wawili, Owono na Matampi ambaye msimu huu amekuwa kipa bora kwa kumzidi nyanda wa Yanga Djigui Diarra.

Ofisa Habari wa Coastal Union, Abbas Elsabri amesema Matampi, bado ana mkataba lakini wamesikia kuwa Simba wana nia ya kuhitaji huduma ya kipa huyo.

“Hatujapata ofa kutoka Simba, lakini nia yao ipo, endapo watakuja hatuna shida na tutakaa mezani na kumaliza dili kama ilivyo kwa beki wetu Lameck Lawi kumuuza kwa wekundu hao wa Msimbazi,” alisema Abbas.

SOMA NA HII  ALICHOKISEMA AJIBU KUHUSU YANGA...KAWAPIGA MKWARA WA 'KUFA MTU' UTADHANI WANACHUKUA 'NDOO'...