Habari za Yanga-Gamondi
Habari za Yanga Leo

GAMONDI AFICHUA MBINU ZA KUIMALIZA AZAM FC… SIENDI KWA KULIPA KISASI

Abubakar June 1, 2024 2:49 pm

KOCHA Mkuu wa klabu ya Yanga SC Muargentina Miguel Gamondi, ameweka wazi mbinu atakayotumia kuimaliza Azam FC, kwenye mchezo wa fainali  wa Kombe la Shirikisho la CRDB,katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Gamondi amefunguka jnsi ambavyo ataingia kwenye mchezo huo, huku akitahadharisha kwamba hawezi kuingia kwa nia ya  kulipa kisasi kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea kupoteza fainali.

 “Kwenye mpira hakuna kulipiza kisasi ukienda kwenye mchezo kwa nia ya kulipiza kisasi hutakuwa na mchezo mzuri, namuheshimu Azam na lazima twende tukacheze mchezo wenye mbinu nzuri ili tuweze kuibuka na ushindi, Yanga na Azam FC wamekuwa na michezo bora msimu huu.”- amesema Miguel Gamondi.

Aidha aliongeza kwa kuelezea jinsi ambavyo jeshi lake, lilivyojiandaa na mchezo huo baada ya kuwasili Ijumaa ya Mei 30, na kufanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo  huo wa fainali.

“Tumepata muda mzuri wa maandalizi na leo (Juni 1) tutafanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wetu wa fainali kesho, Niwapongeze kwa kuchagua Uwanja wa Zanzibar kwasababu ni uwanja mzuri wa kisasa na watu wa Zanzibar pia wataweza kupata nafasi ya kushuhudia fainali hii kubwa” – Miguel Gamondi.

Yanga SC  chini ya Miguel Gamondi imekuwa na msimu mzuri sana, kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, ukiwa ni ubingwa wa mara 30, huku ukisaka kutwaa taji la nane la Kombe la Shirikisho ambao watacheza dhidi ya AZAM FC.

MO DEWJI AKUBALI KURUDI SIMBA…AANZA NA JINA HILI  KUSAJILI SIMBA YAMUWEKEA NGUMU CHAMA… MO HAMUHITAJI TENA